Na Andrew Chale
KUNDI la Dar Modern Taarab na Nadd Ikhwan (Malindi), wanatarajiwa kutoa burudani ya aina yake katika onesho maalumu la ‘Usiku wa Mwambao Asilia’, ndani ya ukumbi wa Travertine, Magomeni jijini Dar es Salaam, Aprili 19.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mlezi wa Heshima wa kundi la Dar Modern Taarab, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Fabak Fashions, Asia Idarous Khamsin, alisema wadau wa muziki wa taarabu watafurahia usiku huo wa Mwambao Asilia kutoka kwa wanamuziki nguli wa miondoko hiyo hapa nchini na visiwani.
“Usiku wa Mwambao Asilia, utasheheni magwiji wakongwe wa muziki wa taarabu nchini, kutoka kundi la Dar Modern Taarab na Nadd Ikhwan, ambao wataporomosha nyimbo za taarabu asili za zamani na za sasa,” alisema Asia Idarous.
Aliongeza kuwa, pia usiku huo utapambwa na ‘surprise’, ikiwemo watu mbalimbali kupita kwenye zuria jekundu ‘red carpet’ na kupiga picha za ukumbusho na mastaa watakaohudhuria usiku huo.
Alisema katika usiku huo, kiingilio kitakuwa ni sh 10,000 ambako tayari tiketi zimeshaanza kuuzwa sehemu mbalimbali.
Asia, alizitaja sehemu hizo kuwa ni pamoja na duka la Fabak Fashions, Regency Park Hotel Mikocheni na Dar Modern Taarab Hall Magomeni Ifunda. Onyesho hilo pia limedhaminiwa na Times FM, Fabak Fashions na www.nakshi255.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...