Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba akiongea na Mkuu wa Masoko wa Vodacom Kelvin Twissa na Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Rosalynn Mworia. Twissa na Mworia walitembeela vyombo vya habari vilivyo chini ya Clouds Media Group katika ziara ya akwaida ya kuimarisha uhusiano.
 Muongoza Matangazo wa kituo cha Radio Clouds na Clouds TV Barnabas Madili akionyesha namna kazi ya kuongoza matangazo inavyofanyika wakati Mkuu wa Masoko wa Vodacom Kelvin Twissa(wa kwanza kushoto) na Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Rosalynn Mworia walipotembelea vyombo vya habari vilivyo chini ya Clouds Media Group. Wa tatu kushoto ni  Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba.
 Waendeshaji wa kipindi cha Morning Choice kinachorushwa na kituo cha Radio cha Choice FM Baby Kabai (kulia) na Evans Bukuku wakionesha manjonjo kwa Mkuu wa Masoko wa Vodacom Kelvin Twissa na Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Rosalynn Mworia (hawapo pichani) walipotembelea vyombo vya habari vilivyo chini ya Clouds Media Group. 
 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya New Habari Corporation Hussein Bashe(kulia)akiwaonesha Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia(katikati) na Meneja Uhusiano  kwa Umma wa Kampuni hiyo Matina Nkurlu moja ya magazeti yanayochapishwa na kampuni yake wakati maofisa hao walipotembelea ofisi za Magzeti ya Mtanzania zilizopo Sinza jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kukuza uhusiano miongoni mwa kampuni hizo.Wa kwanza kulia ni Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mtanzania  Dennis Msacky.
Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia  (katikati) na Meneja Uhusiano  kwa Umma wa kampuni hiyo Matina Nkurlu  wakimsikiliza kwa umakini Mkurugenzi  Mtendaji wa New Habari Corporation Hussein Bashe( kulia) akiwalezea mfumo wa uchapaji magazeti. Maofisa hao wa Vodacom walitembelea ofisi za New Habari Corporation zilizopo Sinza jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kukuza uhusiano kati ya kampuni hizo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...