Msemaji wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Bw. Assah Mwambene (kushoto) akizungumza na wahariri wa Gazeti la Jamhuri Bw. Deodatus Balile, Muhariri Mtendaji (katikati) na Bw. Manyerere Jackton , Naibu Muhariri Mtendaji (kulia) alipotembelea Ofisi za gazeti hilo mtaa wa Samora leo jijini Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa watendaji wa Idara ya Habari kuvitembelea vyombo vya habari kwa lengo la kuimarisha ushirikiano na kutatua changamoto zinazoikabili tasnia ya Habari nchini.
Muhariri Mtendaji wa Gazeti la Jamhuri Bw. Deodatus Balile (kulia) akizungumza jambo na viongozi wa Idara ya Habari waliotembelea ofisi za gazeti hilo leo jijini Dar es salaam. Kutoka Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari-Usajili wa Magazeti Bw. Raphael Hokororo,Afisa habari wa Idara ya Habari Bi. Jovina Bujulu na Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji wa Serikali Bw. Assah Mwambene.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari-Usajili wa Magazeti Bw. Raphael Hokororo akifafanua utaratibu wa utoaji wa vitambulisho kwa waandishi wa habari (Press Card) na namna Idara ya Habari inavyozingatia kigezo cha elimu cha taaluma ya Habari katika kutoa vitambulisho kwa waandishi wa Habari (Press Card) hapa nchini.

Na. Aron Msigwa –MAELEZO.

Vyombo vya habari nchini vimeaswa kutoa kipaumbele kwa habari zinazojenga jamii kwa kuihamasisha kushiriki katika miradi mbalimbali ya maendeleo, kudumisha uzalendo  na kuepuka habari zinazoweza kusababisha mgawanyiko  na chuki katika jamii.

Wito huo umetolewa leo jijini Dar es salaam na Msemaji wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Bw. Assah Mwambene  alipotembelea ofisi za gazeti la Jamhuri zilizoko mtaa wa Samora  jijini Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa Idara hiyo kuvitembelea vyombo mbalimbali vya habari nchini kwa lengo la kukuza ushirikiano na kujadili changamoto mbalimbali za tasnia ya habari hapa nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...