Na Abdulaziz Video, Lindi
Mfuko wa Afya Ya Jamii (CHF)Kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoa
wa Lindi wamewezesha kupimwa kwa Afya za Madereva Boda boda wa kata
ya Kiwalala wilayani Lindi baada ya kufuzu mafunzo ya Udereva.
Mafunzo yaliyotolewa chini ya Mpango shirikishi wa Polisi Jamii Mkoani Humo.
Akiongea na madereva Boda boda mara baada ya kuwatunuku vyeti vya
kufuzu mafunzo hayo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi,Kamishna
Msaidizi Renatha Mzinga ametoa wito kwa wahitimu hao kujali afya zao
kila wakati ambapo aliwahimiza kujiunga na mfuko wa Afya ya jamii ili
kupunguza gharama za Tiba kwa Mwaka.
Aidha Kamanda Mzinga aliwataka kutii Sheria za Usalama barabarani na
kuacha kuendeshwa na Abiria anaemchukua Kwa Usalama wa maisha yao
'Najua sasa ni madereva makini baada ya kupewa mafunzo haya na leo
kuwakabidhi vyeti vyenu ninahakika sasa utoendeshwa na abiria wako
fuata sheria kila wakati na ujenge Tabia ya ya urafiki na askari
tofauti na ilivyo kwa madereva wengi kuogopa askari kwa kuwa wanavunja
sheria kwa makusudi"alimalizia Kamanda Mzinga
Awali Meneja wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoa wa Lindi,Fortunata
Kullaya alieleza kuwa kupitia Mpango wa CHF tayari ofisi yake imeanza
Utaratibu wa kuyafikia makundi mbalimbali katika Programu ya Kata kwa
kata ambapo utoa vipimo Bure kupitia madaktari Bingwa wanaoongozana
nao
"Mfuko wa Chf sasa ndio mkombozi wenu ndugu zangu kwa kuwa unajiunga
kwa pesa ndogo na unatibiwa kwa watu 6 wa kaya moja kwa Mwaka tumieni fursa
hii muhimu na kama ulivyoona leo tumeamua kuja kuwapima Bure ili nanyi
mjue afya zenu nah ii itasaidia kupata Tele kwa tele katika zahanati
zenu toka serikali kuu"Alisema Kullaya'
Jumla ya waendesha Bodaboda 29 waliohitimu mafunzo ya kuendesha
bodaboda walikabidhiwa Vyeti na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi na
baadae kupata Fursa ya kupimwa magonjwa mbalimbali na kupata Ushauri
wa Afya chini ya Mpango wa Kuhamasisha Jamii Kujiunga Na CHF pamoja na
Tiba Kwa Kadi Mkoani Lindi
Baadhi ya waendesha Bodaboda wa kata ya Kiwalala wakimsikiliza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi(hayupo Pichani)katika hafla fupi ya kukabidhiwa Vyeti baada ya kuhitimu mafunzo ya Udereva
Mwendesha Bodaboda Bw Daudi Nanjeka Hamis akipimwa Afya yake katika kampeni inayoendeshwa na Mfuko wa Afya Ya Jamii(CHF) ya upimaji wa hiari iliyofanyika katika hafla ya kukabidhi vyeti kwa
wahitimu
Meneja wa Nhif/chf mkoa wa Lindi,Bi Fortunata Kullaya akitoa elimu ya kujiunga kwa mfuko wa afya ya jamii kwa waendesha bodaboda waliohitimu,Kushoto ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Lindi na Afisa mtendaji wa kata ya Kiwalala Lindi
![]() |
Kamanda wa polisi mkoa wa Lindi,Maafisa wa jeshi hilo na Meneja wa Bima ya afya na waendesha bodaboda katika picha ya pamoja |
Kamanda wa Polisi mkoa wa Lindi akikabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo hayo kwa Mwenyekiti wa waendesha bodaboda Bw Saidi Mchinga katika hafla iliyofanyika katika ofisi ya kata ya Kiwalala wilaya ya Lindi
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...