Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa , Dkt Agnes Kijazi
amefungua rasmi warsha ya matumizi ya mfumo wa GEOCLIM katika
hoteli ya Blue Pearl jijini Dar es Salaam. Warsha hii imeanza rasmi tarehe 8
na itaendelea hadi tarehe 12 Aprili 2014.
GeoCLIM ni mfumo unaosaidia kutoa takwimu za uhakika za taarifa za hali
ya hewa kwa kipindi cha miaka mingi (muda mrefu), kwa kuziweka taarifa
hizo katika mfumo uliorahisi kutumia (gridded)
Dkt Kijazi alisema lengo la warsha hiyo ni kuongeza uelewa wa ukusanyaji
wa takwimu za hali ya hewa za muda mrefu kwa kutumia mfumo wa
GeoCLIM.
Hivyo kusaidia Mamlaka kutoa takwimu za mabadiliko ya hali
ya hewa kwa wakati katika kusaidia sekta mbalimbali kama vile kilimo,
ujenzi, nishati, maji, n.k.
Aliongezea kusema mfumo huu unatarajiwa
kuongeza uwezo wa Malaka katika uchambuzi wa taarifa za hali ya hewa na
hivyo kukabiliana na majanga yatokanayo na mabadiliko ya hali ya hewa
(Climate Change) nchini. Mwisho alisema anatarajia washiriki wa warsha
hiyo wataweza kuutumia vyema mfumo huo ambao ni muhimu sana kwa
maendeleo ya nchi yetu.
Dkt Kijazi aliwashukuru ICPAC na mradi wa PREPARED kwaajili ya
kuandaa na kufadhili warsha hiyo ya mafunzo. Kwa watumishi wa Mamlaka
ya Hali ya Hewa.
Imetolewa na Monica Mutoni;Ofisi ya Uhusiano Mamlaka ya Hali ya
Hewa
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...