WAREMBO wapatao 16 tu ndio watakaoshiriki kwenye kinyang’anyiro cha kumtafuta Miss Tabata 2014 ambalo limepangwa kufanyika Juni 6 katika ukumbi wa Da’ West Park.

Mratibu wa shindano hilo Joseph Kapinga alisema jana kuwa warembo hao wamepatikana baada ya kufanya mchujo iliyojumuisha warembo 40.

Kapinga aliwataja warembo watakaoshiriki kuwa ni Esther Frank Kiwambo (20), Mercy Mathias Kazula (19), Lydia Charles (22), Nuru Omary Athumani (19) na Happyclarrice Wilson Mbahi (19).

Wenine ni Evodia Peter (22), Fatma Hussein Ismail (20),  Ambasia Lucy Mally (22), Angle Kashaga (22), Faudhia Hamisi Feka (21), Najma Charles Mareges (19), Lightnes Olomi (18), Husna Ibrahim (19), Ramta Mkadara (20) , Marry Henry (22) na Mariam Shwaib Hussein (19).

Warembo  hao watachuana vikali kutaka kumrithi Dorice Mollel ambaye anashikilia taji hilo. Dorice pia ndiye anayeshikilia taji la Miss Ilala.

Kapinga alisema kuwa warembo hao kujifua kila siku katika ukumbi wa Da’ West Park chini ya waalimu Neema Mchaki na Pasilida Mandali.

Mratibu huyo alisema fainali hiyo itasindikizwa na aina mbali mbali ya burudani ikiwemo wasanii kutoka nje ya nchi.Warembo watano kutoka Tabata watashiriki kwenye shindano la kanda ya Ilala, Miss Ilala baadaye mwaka huu.

Miss Tabata inadhaminiwa na Zanzi, Redds, Freddito Entertainment, CXC Africa, Saluti5, Brake Point na Integrated Communications.Miss Tabata inaandaliwa na Keen Arts na Bob Entertainment.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...