Afisa mtendaji Mkuu Airtel Africa Christophe Soulet akikata utepe kuzindua rasmi duka la Airtel lililopo mlimani city jijini Dar es Saalam.wakishuhidia, wapili ni Andre Beyers Afisa mkuu wa masoko Airtel Afrika akiwa na meneja wa duka Wahida Saleh na Sunil Colaso Mkurugenzi Mkuu Airtel Tanzania.
Afisa mtendaji Mkuu Airtel Africa Christophe Soulet akikata utepe kuzindua duka la Airtel lililopo mlimani city jijini Dar es Saalam.wakishuhidia, wapili ni Andre Beyers Afisa mkuu wa masoko Airtel Afrika akiwa na meneja wa duka Wahida Saleh na Adriana Lyamba Mkurugenzi wa kitengo cha huduma kwa wateja Airtel Tanzania.
Afisa mtendaji Mkuu Airtel Africa Christophe Soulet na Afisa mkuu wa masoko Airtel Afrika Andre Beyers wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Airtel katika duka la mlimani City mara baada ya uzinduzi rasmi wa duka hilo lililofanyiwa matengenezo na kuwa la kisasa zaidi
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania,Beatrice Singano Mallya akipata maelezo ya huduma za Airtel kutoka kwa wafanyakazi wa Airtel katika duka la mlimani City mara baada ya uzinduzi wa duka hilo lililofanyiwa matengenezo na kuwa la kisasa zaidi.
Airtel Tanzania mwishoni mwa wiki hii imezindua duka la Mlimani City baada ya kulifanyiwa  matengenezo na kulipatia sura ya kisasa zaidi. Uzinduzi huu ni kielelezo cha kampuni hiyo  kutoa huduma bora za simu kwa wateja wake

 Akiongea wakati wa uzinduzi Christophe Soulet, Afisa Mtendaji Mkuu Africa alisema” Airtel tunaamini katika kutoa huduma bora za kisasa zinazoendana na mahitaji ya wateja wetu huku tukiwapa uzoefu wa pekee katika huduma zetu.  Mpango huu wa kuboresha maduka yetu unafanyika katika masoko yetu yote yaliyoko barani Afrika na Leo ninayofuraha kuzindua duka hili la kisasa lijulikanalo kama Express shop hapa nchini Tanzania. Duka hili la kisasa linathibitisha  dhamira yetu ya kutoa huduma bora Tanzania na Afrika kwa ujumla

Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa Airtel Bwana Sunil Colaso  alisema” duka hilo ni la kwanza kuzinduliwa kwani tunabadilisha maduka yetu yote nchi nzima na kuyafanya yawe na mtazamo mpya na wa kisasa zaidi. Duka hili limetengenezwa na kuhakikisha mteja ataweza kupata huduma kwa haraka , kwa usalama bila usumbufu wowote

Aliongeza kwa kusema Airtel inapenda kuwahakikishia wateja kupata huduma bora wakati wote na pia kupata simu za aina mbalimbali ambazo zitapatikana katika duka hilo jipya la Mlimani City.

Kwa kupitia mtandao wetu mpana ulionea zaidi tunawahakikishia wateja wetu huduma bora za kisasa, za uhakika jijini Dar es salaam

Duka la Mlimani City litaendelea kuuza bidhaa mbalimbali kama vile modem na simu za aina mbalimbali ,  wateja watapata huduma ya Airtel money kwa usalama zaidi , kuunganisha na huduma za simu za malipo ya mwenzi na ya awali , pamoja na huduma za internet na kuunganishwa na mtandao  na kuperuzi kwenye internet , kununua muda wa maongezi pamoja na huduma nyingine nyingi.

Airtel Tanzania inaendele kuboresha huduma zake kwa wateja ambapo inaendele kuboresha maduka yake nchini nzima kwa mwaka huu wa 2014.  Mpango ni kuwafikiwa wateja wengi zaidi na kuboresha huduma zake kupitia maduka yake yote yaliyoko nchi nzima. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...