DSC_0083
Mshehereshaji ambaye ni Mwanakamati ya maandilizi ya maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2014, Usia Nkhoma Ledama akiwatambulisha baadhi ya waandishi wa habari wakongwe (hawapo pichani) kwa mgeni rasmi Jaji Mstaafu Mark Bomani.
(Picha zote na Zainul Mzige).

Na Mwandishi wetu
Jaji Mstaafu Mark Bomani amesema lengo la mchakato wa Katiba ni kuhakikisha kwamba Tanzania inapata Katiba ambayo ni bora zaidi kuliko zote itakayoshughulikia changamoto na kuweka mazingira ambayo yatamrahisishia maendeleo mwananchi kwa haraka.
Akitoa risala katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani leo katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC jijini Arusha, Jaji Mstaafu Mark Bomani, amesema jukumu la mwanahabari ni kuwaelimisha baadhi ya wabunge wa Bunge Maalum la Katiba ambao hawana uelewa mkubwa na mchakato wa Katiba hawajui maana halisi ya Katiba mambo ambayo yanasababisha kujadili Katiba hiyo kwa maneno mabaya, kutishiana, matusi na kejeli.
DSC_0171
Baadhi ya waandishi wa habari wakongwe (Ma-veterans) wakimsalimia mgeni rasmi.
“Zoezi la mchakato wa Katiba ni kubwa na wabunge wengi wa Bunge Maalum la Katiba hawaelewi wajibu wao katika kuijadili Katiba hiyo matokeo yake ndio hayo wanayoshuhudia Watanzania”.
Mara nyingi Watanzania wameshuhudia mijadala ya kejeli, malumbano, matusi, kudharauliana pale hoja zinapojengwa na upande ambao haukubaliki na upande mwingine jambo ambalo limewavunja moyo Watanzania na kutokuwa na imani ya kupata Katiba inayolenga kumlinda mwananchi.
Jukumu la wanahabari ni kutoa elimu ya kutosha kuhusu yaliyomo katika Katiba Mpya na kuandika habari za maendeleo ili majadiliano yatokanayo yawe endelevu yamtendee haki mwananchi wa kawaida kwa lengo la kuboresha maisha yao.
DSC_0077
Meza Kuu, kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Elimu, Sayansi na Mawasiliano ya Umoja wa Mataifa (UNESCO) Bw. Abdul Wahab Coulibaly, Mkurugenzi wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF) Bw. Ernest Sungura, Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Bw. John Mongela, Mgeni rasmi Jaji Mstaafu Mark Bomani, Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA-TAN), Bw. Mohamed Tibanyendera, Rais wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Bw. Kenneth Simbaya na Meneja Utafiti na Ushapishaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Bw. John Mirenyi.
“Inasikitisha kuona kuwa hali ya Mtanzania inazidi kudidimia au kubaki pale pale katika sehemu nyingi hasa vijijini katika kipindi cha miaka 40 iliyopita kwa kukosa fursa muhimu za maendeleo na viongozi hawalioni hilo”, amesema Jaji Mstaafu Mark Bomani.
Wakati huo huo mgeni huyo rasmi amekemea tabia ya kuandika habari za kuwasifu viongozi na kupokea Rushwa hali iliyojitokeza katika miaka ya hivi karibuni na kusema kwamba ni fedhea kwa tasnia ya habari kutofuata maadili ya uandishi.
Amesema kwamba nchi itaendeshwa kwa kusimamia haki na ukweli na kuwataka wanahabari wasichoke kuisimamia haki na uhuru wa nchi yao bila woga kwani bila kufanya hivyo nchi itaongozwa kiimla.
DSC_0348
Mgeni rasmi Jaji Mstaafu Mark Bomani, akitoa risala wakati wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2014 yaliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa AICC jijini Arusha mwishoni mwa juma.
“Kuna tabia ya vyombo vya habari ya vyombo vya habari kununuliwa ili visiandike au kufichua maovu ni fedhea kwani vyombo vya habari ni kioo cha jamii”.
Akizungumzia kuhusu sheria za habari za mwaka 2007 na 2008, Jaji Mstaafu amesema ni aibu kuona mswaada wa sheria ya habari umekwama kwa zaidi ya miaka 10 kwa sababu ambazo hadi leo hazijaeleweka.
Amewataka waandishi wa habari wasikate tamaa na badala yake waendelea na kupambana kuhakikisha kwamba harakati za kupata Sheria ya Haki ya Kujua inafanikiwa ili kupunguza matukio ya manyanyaso, kupigwa, kuteswa, kufungwa kwa vyombo vya habari na kuuwawa.
“Haki haiyombwi simamieni Haki zenu na songeni mbele”, ameongeza Jaji Bomani. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 06, 2014

    Waandishi wengi viwango vyao viko chini sana. Ukitaka kuthibitisha subiri uone jinsi watakavyoandika habari za bajeti itakayosomwa Bungeni ya mwaka 2014/2015. Wanabakia tu kuandika mara huyu kasema hivi mara huyu kasema hivi. Shida yao kubwa hawafanyi utafiti binafsi. Utakuta wanaandika bila marejeo ya kisayansi. Hakuna jedwali,linaloonesha ukuaji wa uchumi, matumizi, ukusanyaji wa kodi, madeni. Hivi vyote vinahitaji uandishi wa kitaalamu ambao waandishi wetu hawana, na kama wanao hawautumii. Toeni takwimu za kitaalamu ili kuelimisha watu acheni kurukia mawazo mara ya mhadhiri wa chuo fulani, mara mwana siasa...hayo ni mengineyo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...