Ankal akiwa na mpiga saxophone maarufu nchini Tanzania Akuliake Salehe a.k.a. "King Maluu"   alipogongana nae akitumbuiza kwenye hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es salaam jioni ya leo akiwa na Furaha band chini ya Mohamed Amon (anaepiga gitaa). King Maluu, ambaye alitamba sana enzi za Maquis du Zaire, Orchestra Safari Sound na Wazee Sugu, hivi sasa ni lulu katika tasnia ya Bongo Flava ambapo amekuwa akiwapiga taffu vijana wa kizazi kipya na saxophone yake. Mfano ngoma ya "Number one" ya Diamond na pia ya Ommy Dimples ya "Tupogo".
Sikiliza King Maluu anavyochambua saxophone kama karanga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 18, 2014

    Dah! Ankal namzimia sana mzee huyu asiyezeeka. Nangoja kwa hamu kusikia soundz zake. Pliiis weka fasta kabla sijaenda shift ya box plisssss!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 18, 2014

    Ankali hilo shati wapi hiyo... Abuja?

    ReplyDelete
  3. Hivi huyu ndo alikuaga kyauri voice??

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 18, 2014

    halafu ankal kaadimika sana siku hizi. unajua tukiona face yako humu tunafarijika mno. pamoja na wazifa ankal usitusahau bhana! Tumaiss ze fulanazzzzz, konozzzzzz, nondozzzzz na vitu kibao. wape lekcha vijana wako walete mambozzzz, japokuwa hivi sasa globu yetu imekuwa kubwa kiasi hata msindani wa karibu haonekani. nyuzzz za kila pembe ya nchi kila dakika. hongera and keep it up ze libenekezzzzzz....

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 18, 2014

    Dah! Ankali nimerudi tena na shukrani kwa kunihudumia kabla ya kwenda kula box. huyu King Maluu ni noma! Asante Ankal, acha niwahi shifti. huku kazini haturuhusiwi kugusa mtandao wakati wa kazi, yaani hata simu hupokei. Namiss Bongo wallahi

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 19, 2014

    issah jamaa alishapigia band ya kyauri voice na vumbi nyuma?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...