AzamTV leo wamezindua mashindano yatakayowahusisha wapenzi wa kandanda yatakayojulikana kama KWETU HOUSE. Mashindano haya ambayo ni mara ya kwanza Tanzania yatashirikisha wapenzi na mashabiki wa mpira wa miguu ambapo watu kumi wa 10 wa timu mbalimbali watachaguliwa na kuishi katika nyumba moja kwa muda wa siku 3 wakionyesha ni jinsi gani wao ni mashabiki namba mmoja kwa timu zao .
Akizindua mashindano hayo, Mkurugenzi mtendaji wa AzamTV, bwana Rhys Torrington alisema: Lengo kuu la kufanya shindano hili ni kuamsha hisia za mashabiki wa soka na kuonyesha umuhimu wa kuthamini mashabiki kwa sababu bila wao mpira wa miguu usingekuwepo leo hii; wakati huo huo ni kuwaletea watazamaji vipindi vinavyoburudisha na kuelimisha.
Mashindano haya yametokana na ubunifu wa wafanyakazi wa Azamtv ambapo hiki ni kipindi kimojawapo kitakachofuatiwa na vingine vingi ambavyo viko ndani ya maandalizi kupitia kampuni ya Uhai Production ambayo ni kampuni mama ya AzamTV; aliongeza bwana Wasiwasi Mwabulambo ambaye ni mratibu wa mashindano hayo. Wanaoruhusiwa kushiriki mashindano haya ni wanaume wenye umri wa miaka kumi na nane (18) na kuendelea.
Wakiwa ndani ya jumba la KWETU HOUSE washiriki wataenguliwa kila siku ya jumapili mpaka kubakia washiriki watatu ambapo mmoja wao atajinyakulia kitita cha shilingi milioni kumi (10).
Usaili wa shindano hili utafanyika siku ya jumamosi tarehe 24/05/2014 uwanja wa Leaders club, kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 11 jioni. Usaili utakuwa ni bure. Pia mashabiki wanaweza kujisajili kwa kutuma video zao fupi kwenda kwenye whatsApp number 0759 38 65 68 nakuonyesha ushabiki wao wa dhati.
Watakaochaguliwa watatangazwa tarehe 27/05/2014 ambapo wataingia ndani ya jumba la KWETU HOUSE tarehe 30/05/2014; na mshindi atapatikana tarehe 27/06/2014.
Shindano hili limedhaminiwa na Azam Energy Drink kwa ushirikiano wa Channel Ten, Magic Fm na Times Fm.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...