Barabara ya Kijichi – Mbagala Kuu, ndani ya jiji la Dar es Salaam kama ilivyokutwa jana na Mdau Nathan Mpangala. Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Butiama, Bw. Haji Mgaya, alisema, dhahma hiyo ni ya muda mrefu na Manispaa ya Temeke ina taarifa hiyo kwa kupindi chote hivyo,lakini mpaka leo iko kimya tu. 
Hapa dereva ‘akilala’ tu, kilio kitongoji kizima zikifuatiwa na salamu za rambirambi nyiiingi toka kwa viongozi.
Inawezekana Manispaa ya Temeke haina picha halisi ya hatari hii!!!
Halafu hapo hapo ni kituo cha daladala! Manispaa ya Temeke hata alama za hatari pia hakuna?
Kwa maana nyingine gari ikitumbukia hapa, mpaka ije ijikite chini itakuwa imepiga samasoti za kutosha!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 21, 2014

    Hii iko sawa sawa na ya Tabata Kimanga

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 21, 2014

    yaani manispaa ya temeke uozo mtupu wadau hapo kama lumo kona barabara ime momonyoka hakuna ufumbuzi wowote karibu miezi miwili sasa ankal we njoo mwenyewe ujionee panda gari za machimbo shuka lumo kona

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 21, 2014

    Yakitokea maafa hapo tutasema ni mipango ya Mungu!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 22, 2014

    Jamani ata sisi wananchi wa Kitunda Shule mpaka Mwanagati shule ya Mzinga tunalia na Barabara yetu ni mbaya zaidi ya hii.

    Mbunge wetu amelala, Madiwani wamelala yaani tabu tupu. Tunaomba chama chetu tunachokipenda cha CCM msiwape nafasi hawa wagombea wa sasa tuletee wengine maana wakirudia kugombea hatuwapi wao kabisa kura...Wapigeni chini wanaangusha chama chetu kikubwa na kizuri!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...