Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akishirikiana na watendaji wa Wizara ya Ujenzi na TANROADS akishinda siku nzima na hata kukesha usiku mzima aliweza kushishiriki kikamilifu kama waziri mwenye dhamana kurejesha huduma za usafiri wa barabara zilizojifunga kutokana na kusombwa/kuharibiwa kwa madaraja muhimu yanayouunganisha mji wa Dar es Salaam na maeneo mengine hasa mikoa jirani. Maeneo yaliyoharibiwa ni daraja la Mpiji (Bagamoyo), Mzinga (Mbagala, Kongowe), daraja la Mto Mtokozi (barabara ya Kongowe – Mjimwema – Kigamboni) na Ruvu (Barabara ya Morogoro).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 01, 2014

    Yaani ingawa sina chama lakini nimeguswa sana na uchapa kazi wa Mh.Waziri Magufuli. jamaa ingawa ni waziri lakini yupo usiku na mchana kuhakikisha dalaja linajengwa, safi sana. Sikumbuki uchapakazi wa kiongozi yoyote tokea enzi ya Sokoine. Mungu akulinde Magufuli, wewe ni zaidi ya Jembe kwa kuwajali watu wako.

    *Mmmbongo Chiberia*
    Diaspora daima.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 01, 2014

    Nchi yetu ikipata viongozi wa juu 5 tu wenye moyo kama wa Mheshimiwa Magufuli shida inatuisha..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...