Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji nchini (EPZA), Dkt. Adelhelm Meru (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dkt. Hassan Mshinda wakitia saini makubaliano ya uanzishaji na uendelezaji wa eneo maalumu la hekari 238 Bagamoyo kwa ajili ya kuendeleza teknolojia ya habari na mawasiliano nchini. Waliosimama ni Afisa wa EPZA, Bi. Sarah Patric na Mwanasheria wa Tume hiyo, Bi. Zainab Bakari (kulia). Tukio hilo lilifanyika jijini Dar es Salaam Jumatatu wiki hii.



 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji nchini(EPZA), Dkt.Adelhelm Meru (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia(COSTECH), Dkt. Hassan Mshinda wakibadilishana nyaraka baada ya kutia saini makubaliano ya uanzishaji na uendelezaji wa eneo maalumu la hekari 238 Bagamoyo kwa ajili ya 
kuendeleza teknolojia ya habari na mawasiliano nchini. Tukio hili lilifanyika jijini Dar es Salaam Jumatatu wiki hii. 
---------------------------------------------
Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji nchini (EPZA) imefikia makubaliano na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kuanzisha na kuendeleza eneo la teknoloji ya habari na mawasiliano (TEHAMA) nchini.
Eneo hilo linalenga kuvutia kampuni za ndani na nje ya nchi kuja kuwekeza kwa ajili ya kukuza sekta hiyo.
Utiaji saini huo ulifanywa na Mkurugenzi Mkuu wa EPZA, Dkt. Adelhelm Meru na mwenzake wa COSTECH, Dk. Hassan Mshinda jumatatu hii jijini Dar es Salaam.
Akizungumza baada ya utiaji saini huo, Dk. Meru aliwambia waandishi wa habari kuwa makubaliano hayo ni muhimu kwa maendeleo ya nchi.
“Taasisi hizi mbili za serikali leo zimeingia katika hatua muhimu ya kuanzisha na kuendeleza eneo muhimu la TEHAMA hapa nchini,”alisema Dkt. Meru.
Alisema makubaliano hayo yamelenga kulitumia eneo maalumu la uwekezaji la mamlaka hiyo lililo Bagamoyo kwa ajili ya nia hiyo.
Likimalizika, eneo hilo linatarajiwa kuwa kituo kikubwa cha maswala ya TEHAMA kwa nchi za Afrika Mashariki na kati.
Alisema eneo hilo lenye jumla ya hekari 238 litaendelezwa kwa ushirikiano wa tasisi hizo mbili kujenga miundombinu ya maji, barabra  na umeme ili kuyavutia makampuni makubwa duniani yakiwemo ya DELL, IBM MICROSOFT na HP kuwekeza.
“Bagamoyo itakuwa kitovu cha maswala ya TEHAMA na hili ni jambo kubwa kwa nchi yetu hasa katika kufikia Matokeo makubwa (BRN),”aliongeza kusema, Dk. Meru.
Alisema pamoja na kwamba miundombinu hiyo inatarajia kugharimu Tsh. Bilioni 50, lakini faida ya kuanzisha na kuendeleza eneo hilo ina manufaa makubwa kuliko gharama hiyo.
Alisema makampuni hayo yataleta teknolojia, mitaji mikubwa na matarajio ni kwamba eneo litatoa ajira zaidi ya 100,000 na kuwa hiyo ndiyo sera ya serikali katika harakati za kukuza ajira hapa nchini.
Kwa upande wake, Dk. Mshinda aliita hatua hiyo kama hatua muhimu nay a kihistoria katika maendeleo ya TEHAMA hapa nchini.
“Eneo hili pia litakuwa ni fursa ya kujenga uwezo wa watanzania katika eneo hili muhimu kwa maendeleo ya nchi,” alisema.
Alisema kwamba eneo hilo litavutia vyuo vikuu, taasisi na kampuni za ndani na nje ya nchi kuja kuwekeza na kwa kufanya hivyo nchi itapata fedha za kigeni.
“Katika kuendeleza miundombinu ya eneo hili tunalenga kushirikiana na sekta binafsi ili kuleta ufanisi zaidi,”alisema.
Alisema tayari wameshazungumza na baadhi ya wawekezaji vikiwemo vyuo vikuu na kampuni kutoka nchi kama Malaysia na India kufanikisha azma hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...