Mkurugenzi mkuu wa benki ya FNB Tanzania Bw. Dave Aitken akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa tawi jipya la Benki hiyo,lililopo Kariakoo jijini Dar es salaam.kushoto ni Msimamizi wa Masuala ya Athari na Tahadhari wa benki ya FNB Tanzania, Bw. Silvest Arumasi, na kulia ni Afisa Msimamizi Mkuu wa fedha wa benki hiyo, Bw. Luke Woodford.
Katika kukuza na kusaidia wafanya biashara wadogo na wakati benki ya FNB Tanzania imefungua tawi jipya la kariakoo, ambalo litakua na kazi ya kutoa huduma za kibenki kwa wafanya biashara wadogo na wakati ijulikanayo kama SME ili kuwainua kiuchumi.
Tawi jipya la Kariakoo limelenga kutoa huduma za kibenki kwa wafanya biashara wa soko hilo na pia kuwasaidia kukuza mtaji pamoja na kufikia malengo yao kibiashara. Kati ya huduma zinazotolewa na tawi hilo ni pamoja na msaada wa huduma za kibenki katika biashara na huduma za kibenki za kimataifa.
Akiongea wakati wa ufunguzi wa tawi hilo Bw. Dave Aitken mkurugenzi mkuu wa benki ya FNB Tanzania alisema, "tunayo furaha kufungua tawi letu jipya la kariakoo ambalo litakua linatoa huduma madhubuti za kibenki kwa wateja wetu ambao ni wafanya biashara kujumuisha wadogo na wafanya biashara wakati. Tumejidhatiti kuwasaidia katika kukuza biashara zao kitaifa na kimataifa tunaamini kukua kwao katika biashara kutakuza uchumi wa nchi pia"
Ikiwa ni mika miwili itu tangu benki ya FNB imeanza shughuli zake lakini imekua ni benki inayoongoza hapa nchini katika kutoa huduma ambazo zinakizi viwango vya ushindani kwa wateja. Pia FNB imeleta mapinduzi ya matumizi ya huduma za kibenki kwa njia ya simu na mtandao kwa wateja wake ili kuhakikisha wateja wananufaika na maendeleo ya teknolojia.
Huduma nyingine za kibenki zitolewazo na benki ya FNB ni pamoja na taarifa za kibenki kwa njia ya mtandao, kulipia huduma nje ya nchi kupitia huduma za SWIFT, taarifa za kibenki kwa njia ya ujumbe wa simu, na matumizi ya kadi za kietroniki (yaani VISA Card) katika kutoa pesa na kulipia bidhaa au huduma. FNB imefanikiwa kuanzisha huduma za kisasa ambazo imetofautisha benki hiyo na benki nyingine zinazotoa huduma hapa nchini.
Kwa upande wa uchumi Bw. Andy Watkins, Mtendaji Mkuu, alisema kuwa uchumi wa Tanzania umekuwa kwa 7% ukilinganisha na miaka iliyopita, ongezeko hilo limetokana na shughuli mbalimbali kama vile uchimbaji wa madini, utalii, viwanda na kilimo. Soko la Kariakoo ni kitovu cha biashara ambapo waingizaji na wasambazaji utumia soko hili kufanya biashara zao, hivyo upatikanaji wa uduma za kibenki kupitia benki ya FNB itawasaidia wafanya biashara kuimalisha maendeleo yao katika ngazi ya mtu mmoja mmoja.
"Tunaamini kuwa huu ndio muda muafaka wa kuwekeza na kukuza msingi wa biashara nchini na ufunguzi huu wa tawi la Kariakoo ni sehemu ya jitihada zinazofanywa na benki ya FNB katika kuakikisha biashar inakua kwa kasi nchini. Na tunawaakikishia kuwa benki ya FNB kupitia tawi la Kariakoo itakuza mahusiano mazuri na wafanya biashara ili kuakikisha wafanya biashara hao wananufaika na huduma zitolewazo na benki," aliongeza.
Lengo la Benki ya FNB ni kuakikisha kuwa benki inakuwa mstari wa mbele katika kukuza sekta za fedha na ina mpango wa kuanzisha huduma nyingine za kisasa na kuleta wataalamu kutoka ukanda wa Jangwa la Sahara katika sekta ya kiklimo na madini ambao watakua chachu ya ukuaji wa uchumi wa nchi.
Katika mwaka 2012 benki ya FNB ilitajwa kuwa ni benki ya ubunifu kutoka na huduma zitolewazo katika tuzo za BAI (Finacle Global Banking Innovation Awards). Tuzo hiyo ilidhiirisha jinsi benki ya FNB ilivyojidhatiti katika uduma zake na ubunifu wake katika utoaji huduma kwa wateja. Ubunifu huo utajionesha pale ambapo benki inaweza kutoa huduma bora na za kisasa kwa wateja ili kuakikisha wateja wanakidhi mahitaji yao.
Tangu mwaka 1874 Benki ya FNB imekuwa ikiendesha shughuli zake katika nchi mbalimbali za ukanda wa Jangwa la Sahara barani Afrika pia inaendesha shughuli zake katika nchi za Zambia, Msumbiji, Lesotho, Swaziland, Botswana na Namibia, ambapo makao yake makuu yapo nchini Afrika kusini. Lengo la benki ya FNB ni kuwa benki inayoongoza barani Afrika.
FNB Tanzania ilianza rasmi Julai 27, 2011, ikiwa na matawi matatu jijini Dar es Salaam ambayo ni tawi la Posta, Quality Centre na Peninsula iliyoko eneo la Coco beach, tawi hili linalofunguliwa leo ni la nne, lakini hata hivyo benki ya FNB inajiandaa kufungua matawi mengine matatu hapa jijini Dar es Salaam ili kukidhi mahitaji ya wateja wake.
Kwa taarifa tembelea tovuti www.fnbtanzania.co.tz au barua pepe info@fnb.co.tz
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...