Mamia ya wakotiliki wamejitokeza kumuaga Askofu wa jimbo la katoliki Dodoma,Mhashamu Baba Askofu Gervas John Nyaisonga ambaye anahamia Mpanda kwa ajili ya kuendelea na kazi Dini.Sherehe hiyo iliyotanguliwa na Ibada ilifanyika katika Kanisa kuu la Mtakatifu Paulo wa Msalaba mkoani Dodoma.

Mgeni rasmi katika sherehe hiyo ambayo alikuwepo Mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pina,alikuwa Kiongozi wa Kanisa Katoliki hapa nchini,Mwadhama Polcarp Kardinal Pengo. Pia sherere hiyo ilihudhuriwa na Askofu mstaafu wa jimbo la Domama Mhashamu Baba Askofu Mathias Isuja.

Katika sherehe hiyo ,Mhashamu Baba Askofu Gervas John Nyaisonga. alizawadiwa vitu mbali mbali zikiwemo fedha taslimu. Mhashamu Baba Askofu Gervas John Nyaisonga anaondoka rasmi Dodoma kuelekea Mpanda Ijumaa tarehe 2 akipitia Tabora. Amehamishiwa kwa kazi za Kichungaji Jimbo la Mpanda.

Pamoja na kuhudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mama Rehema Nchimbi,Papadri na watawa wote wa jimbo la Dodoma kulikuwepo vikundi vya kwaya kutoka makanisa mbalimbali ikiwemo kwaya ya Kanisa analosali Mhe.Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Kwaya ya Shirikisho Hananasifu Dar es Salaam.
Kiongozi wa kanisa Katoliki hapa nchini Mwadhama Polcarp Kardinali Pengo (kulia) akipeana mkono na Askofu Gervas John Nyaisonga.
Mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda akibusu Pete ya Kiongozi wa kanisa Katoliki hapa nchini Mwadhama Polcarp Kardinali Pengo.
Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda akisalimiana na Kiongozi wa kanisa Katoliki hapa nchini Mwadhama Polcarp Kardinali Pengo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...