MFUKO
WA PENSHENI WA LAPF NI MFUKO WA HIFADHI YA JAMII NCHINI TANZANIA WENYE MAKAO
MAKUU YAKE MJINI DODOMA.
.jpg)
IELEWEKE KUWA INGAWA WAHESHIMIWA WABUNGE AU MTU AU TAASISI YEYOYE HAWAZUILIWI KUOMBA MSAADA WA KIJAMII, MH. MBILINYI NA MH. MSIGWA HAWAJAWAHI KUWASILISHA MAOMBI NA HAWAJAWAHI KUPEWA MSAADA WOWOTE NA LAPF.
AIDHA LAPF INAKANUSHA HABARI ZILIZOTOLEWA KATIKA GATEZI LA MTANZANIA LA TAREHE 26 MEI 2014 TOLEO NA. 7472 KUWA WAHESHIMIWA WABUNGE NI WASUMBUFU NA KUMFANYA MKURUGENZI MKUU ASIENDE BUNGENI.

AIDHA, SI KWELI PIA KWAMBA LAPF HAISHIRIKI KATIKA BAJETI YA OFISI YA WAZIRI MKUU KWANI MFUKO HUU UKO CHINI YA OFISI YA WAZIRI MKUU TAMISEMI NA INASHIRIKI KATIKA VIKAO HIVYO.
LAPF INAPENDA KUWAJULISHA UMMA WA WATANZANIA KUWA MFUKO HUTOA MISAADA YA KIJAMII KWA KUZINGATIA MPANGO NA BAJETI ILIYOIDHINISHWA NA KWA KUZINGATIA SERA YA MISAADA YA KIJAMII NA MAOMBI YANAYOWASILISHWA. PIA HAKUNA TAASISI AU MTU BINAFSI INAYOPEWA FEDHA TASLIM ISIPOKUWA MFUKO HUNUNUA VIFAA NA KUWASILISHA MOJA KWA MOJA KWA WAHUSIKA.
MFUKO WA PENSHENI WA LAPF UNAENDESHWA CHINI YA SHERIA
YA LAPF (THE LOCAL AUTHORITIES
PENSIONS FUND ACT NO. 9 OF 2006). SHERIA HII IMEFANYIWA MAREKEBISHO KUKIDHI MAHITAJI YA
SHERIA YA USIMAMIZI WA HIFADHI YA JAMII YA MWAKA 2008 (SSRA) NA KWA
SASA LAPF INAANDIKISHA WANACHAMA TOKA SEKTA ZOTE NCHINI NA JINA LA MFUKO
LILIREKEBISHWA NA SASA LINAJULIKANA KAMA MFUKO WA PENSHENI WA LAPF (LAPF PENSIONS FUND).
SHUGHULI
KUU ZA MFUKO NI PAMOJA NA KUANDIKISHA WANACHAMA, KUKUSANYA MICHANGO, UWEKEZAJI
NA KULIPA MAFAO.
KWA SASA LAPF INATOA MAFAO MBALI MBALI AMBAYO NI MAFAO YA
UZEENI, MAFAO YA MIRATHI, MAFAO YA KUUMIA KAZINI, MAFAO YA UZAZI, MAFAO YA
KUJITOA, MSAADA WA MAZISHI, MIKOPO YA NYUMBA, MIKOPO YA WANACHAMA KUPITIA
SACCOS NA IPO KATIKA HATUA ZA MWISHO ZA KUTOA MIKOPO YA ELIMU KWA WANACHAMA.
PAMOJA
NA MAJUKUMU MAKUU YA MFUKO YALIYOTAJWA HAPO JUU, MFUKO UNASHIRIKI PIA KATIKA
KUISAIDIA JAMII NA HIVYO KUSAIDIA KATIKA KUPUNGUZA UMASIKINI NA KUCHOCHEA
MAENDELEO ( CORPORATE SOCIAL RESPONSIBILITY).
MISAADA
HII INA LENGO LA KUSAIDIA JAMII YOTE YA WATANZANIA YENYE MAHITAJI MBALI MBALI
NA KWA KUTAMBUA KUWA MISAADA HII ITAWANUFAISHA SI WANACHAMA WA LAPF TUU BALI
PIA WANANCHI WOTE.
LAPF
IMEKUWA IKITOA MISAADA YA KIJAMII KATIKA SEKTA MBALI MBALI KAMA VILE AFYA,
ELIMU, VITUO VYA WATOTO YA YATIMA, TAASISI ZA WATU WENYE MAHITAJI MAALUM, SEKTA
YA MICHEZO NA KUSAIDIA MAAFA KWA KUTOA VIFAA MBALI MBALI KAMA MASHUKA, VYANDARUA NA MADAWA, KATIKA ELIMU
KUCHANGIA UJENZI WA MADARASA, UNUNUZI WA MADAWATI NA VIFAA VYA MAABARA. KATIKA
VITUO VYA WATOTO YATIMA LAPF IMEKUWA IKITOA MISAADA YA VYAKULA, MAVAZI NA VIFAA
VYA SHULE. KADHALIKA KATIKA MICHEZO LAPF IMEKUWA IKICHANGIA VIFAA VYA MICHEZO
KAMA JEZI NA MIPIRA.
KWA MIAKA MITATU MFULULIZO MFUKO WA LAPF NDIO UMEKUWA
MDHAMINI MKUU WA MICHEZO YA JUMUIYA YA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU (TUSA) AMBAO NI
WANACHAMA WATARAJIWA WA MFUKO.
KATIKA
MWAKA WA FEDHA 2013/2014 MFUKO WA LAPF UMETOA MISAADA MBALI MBALI KAMA VILE
VIFAA VYA UJENZI CHUO CHA MADAKTARI BUGANDO NA CHUO KIKUU HURIA (OUT).
KADHALIKA
LAPF IMEOTA VIFAA MBALI MBALI VYA SHULE KAMA VILE MADAWATI, TAA ZA SOLA NA
MASHINE ZA FOTOKOPI.
KATIKA
SEKTA YA AFYA LAPF IMETOA MSAADA KWA HOSPITALI NA ZAHANATI MBALI MBALI NCHINI
KWA KUTOA VYANDARUA, MASHUKA, MADAWA, VIFAA VYA MAABARA, TAA ZA SOLA PAMOJA NA
KUCHANGIA MAADHIMISHO YA SIKU YA WAUGUZI DUNIANI.
KATIKA
MICHEZO LAPF IMEENDELA KUWA MDHAMINI WA MICHEZO YA JUMUIYA YA WANAFUNZI WA VYUO
VIKUU (TUSA) NA VIFAA VYA MICHEZO KWA SHIRIKISHO LA SERIKALI ZA MITAA
(SHIMISEMITA).
HII
NI BAADHI TU YA MISAADA AMBAYO LAPF IMETOA KWA MWAKA HUU KWA KUZINGATIA MAOMBI
MBALI MBALI YALIYOWASILISHWA PAMOJA NA BAJETI NA MPANGO WA MFUKO ULIOIDHINISHWA.
KWA MWAKA HUU WA FEDHA, MISAADA YOTE HADI SASA INA JUMLA YA THAMANI YA SHILINGI
MILIONI MIA MOJA NA ISHIRINI. AIDHA, KUTOKANA NA UFINYU WA BAJETI YA MFUKO,
SEHEMU KUBWA YA MISAADA HII NI KATI YA SHILINGI LAKI TANO HADI MILIONI TATU.
MISAADA HII HUTOLEWA MOJA KWA MOJA KWA WALENGWA NA PIA SI FEDHA TASLIMU, BALI
VIFAA HUSIKA.
STAAFU KWA UFAHARI NA LAPF.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...