NENO LA LEO: Luka 6: 27-28  Lakini nawaambia nyie mnaosikia, wapendeni adui zenu,watendeeni mema wale ambao wanaowachukia ninyi.  28 Wabarikieni wale ambao wanawalaani ninyi, Waombeeni wale ambao wanaowaonea ninyi.

TAFAKARI: Neno la leo ni mtihani mkubwa sana manake Bwana Yesu anatuamuru kuwa tuwapende maadui zetu na kuwaombea wale ambao wanatuonea. Kiubinadamu ni kawaida kutaka kulipiza mabaya kwa mabaya. Hiyo ndiyo asili yetu. Lakini sisi Wakristo tunatakiwa maisha yetu yawe ni mafundishona mfano mzuri kwa jamii nzima. 

Mungu anataka maisha yetu yaige mfano wake yeye. Kama yeye anavyotusamehe tukimkosea,basi na sisi tusisite kuwasamehe wale wanaotukosea. Sala ya bwana ambayo tulifundishwa na  Bwana Yesu inasema kuwa “utusamehe makosa yetu, kama nasi tunavyowasamehe wale waliotukosea” . Hapa moja kwa moja tunampa Mungu kipimo cha kupimia jinsi ya kutusamehe. 

Kama husamehe wenzio, usitegemee kusamehewa. Kama unasamehe kidogo, na wewe utasamehewa kidogo. Tunapomsamehe mtu, basi iwe ni kweli na sio unafiki. Unapoonyesha mapenzi hata kwa wale ambao wanakutesa na kukufanyia vitendo vya kidhalimu, Roho mtakatifu atafanya kazi yake na kubadilisha roho za hao watu wagumu.  Kitabu cha  Matayo 6:14  kinasema;  Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao,na baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi.

SALA: Ee Mungu baba wa reheme, tunakuomba utupe roho ya imani na upatanishi. Utusaidie tuweze kuishi  maisha ambayo yatakuwa ni mahubiri ya ushuhuda wetu. Matendo yetu na mienendo yetu idhihirishe kuwa sisi ni wafuasi wako. Utujaze upendo kwa maana ndiyo moja katika zile amri zako kuu mbili. Amen (c) IYK_NENO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...