Rais Jakaya Kikwete  amewasili mjini Kinshasa  Jamhuri ya Watu wa Kongo (DRC) usiku wa kuamkia leo kwa ziara ya kikazi akitokea nchini Nigeria ambapo amehudhuria Mkutano wa Viongozi kuhusu Uchumi barani Afrika.
 Akiwa Kinshasa, leo tarehe 10 Mei, Rais Kikwete amefanya  mazungumzo na Rais Joseph Kabila ambapo wanatarajia kuzungumzia uhusiano baina ya nchi mbili hizi na hali ya kisiasa kwa ujumla katika ukanda wa Jumuiya ya ushirikiano wa Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). 

 Mara baada ya Mazungumzo haya Rais Kikwete ameondoka kuelekea Luanda , Angola kwa ajili ya mazungumzo na Rais Jose Dos -Santos.

   Wakati huo huo, Rais Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Rais Joyce Banda wa Malawi kufuatia kifo cha ghafla cha Balozi wa Malawi nchini Tanzania Flossy Gomile-Chidyaonga kilichotokea tarehe 9 Mei jijini Dar-Es-Salaam. 

 "Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba wa Balozi Chidyaonga, ni huzuni kwetu sote" Rais amesema na kumuelezea Balozi Chidyaonga kuwa alikuwa mcheshi na aliyependa kushirikiana na wenzake kwa moyo mkunjufu. 

 " Ni huzuni zaidi kwetu sote kwakuwa kifo chake kimetokea ghafla mno kwa mtu tuliekua tunashirikiana naye kwa karibu katika juhudi za kukuza na kuimarisha mahusiano baina yetu" Rais amesema na kuongeza kuwa, kifo chake kimetokea wakati tunamhitaji zaidi na hivyo kusababisha pengo kubwa" 

 Rais amemuomba Rais Banda kufikisha salamu zake binafsi na za Watanzania kwa ujumla kwa familia ya marehemu, ndugu, Jamaa na Wamalawi wote kwa ujumla na kumuombea marehemu kwa mwenyezi Mungu, ampe mapumziko mema milele. 

 Imetolewa na; 
Premi Kibanga, 
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi, 
Kinshasa-DRC 10 Mei 14
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa na mwenyeji wake Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Demokrasia ya  Kongo ikulu ya Kinshasa leo.Rais Kikiwete alikuwa nchini DRC kwa ziara ya kikazi ya siku mbili(picha na Freddy Maro)
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagwa na mwenyeji wake Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Demokrasia ya  Kongo ikulu ya Kinshasa leo.Rais Kikiwete alikuwa nchini DRC kwa ziara ya kikazi ya siku mbili
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mwenyeji wake Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Demokrasia ya  Kongo ikulu ya Kinshasa walipokutana kwa mazungumzo

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete alipokuwa  katika mazungumzo na mwenyeji wake Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Demokrasia ya  Kongo ikulu ya Kinshasa leo.Rais Kikiwete alikuwa nchini DRC kwa ziara ya kikazi ya siku mbili. Picha na Freddy Maro

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 10, 2014

    Kwanza nikupongeze Rais kuamua kumtembelea Rais Joseph Kabila. Hii ni nafasi nzuri ya kuimarisha biashara na nchi hii kubwa. Makampuni mengi yafuate mfano wa PTA. Fungueni ofisi DRC. Benki za kitanzania ziende huko kuwasaidia wafanya biashara. Mbona Benki za Kenya zimefungua ofisi Tanzania? Na sisi tuwahimize wafanya biashara wafungue ofisi DRC ili biashara ikue mara dufu. Mbona mheshimiwa hukwenda na kundi la wafanya biashara? Au hiyo inafaa ulaya tu?

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 10, 2014

    Hapo anaonekana JK akimwambia JK, "Tulia kijana na usiwe na wasiwasi PK nimedhibiti pamoja na YK."

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...