Rais Kikwete akiwa na Mbwana Samatta kulia na Thoams  Ulimwengu kushoto mjini Kinshasa leo

RAIS wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete leo amewatembelea washambuliaji wawili Watanzania wanaocheza TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mbwana Ally Samatta na Thomas Emannuel Ulimwengu.
Tovuti ya TPM imeandika kwamba Rais Kikwete aliwatembelea wachezaji hao leo mjini Kinshasa ambako wapo na timu yao kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya DRC dhidi ya mahasimu wao katika mbio za ubingwa AS Vita.
Rais Kikwete aliye ziarani DRC, alikuwa ameambatana na maofisa wawili wa Ubalozi wa Tanzania majira ya Saa 6:15 mchana alipokutana na wachezaji hao pamoja na Mwenyekiti wa klabu yao, Moses Katumbi.
Rais Kikwete alikuwa  Kinshasa  kwa ziara maalum ya Siku mbili  juu ya ushirikiano wa DRC na Tanzania, ambako alikutana na Rais  Joseph Kabila.
Kikwete alitumia robo saa kuzungumza na akina Samatta katika hoteli ya Congo River, ambako wameweka kambi kwa ajili ya mechi ya kukata na shoka kesho.
Rais Kikwete aliwakumbusha Samatta na Ulimwengu kwamba, Watanzania wanajivunia kuwaona wakiwa na jezi za TPM na kwamba wao ni tegemeo la timu ya taifa, Taifa Stars kwa sasa.
CREDIT:BIN ZUBEIRY

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. JK ama kwa hakika wewe ni mtu wa kipeke Tanzania Kuwahi kutokea. Mengi umefanya Na utabakia katika kumbukumbu zetu daima . Mungu akubariki na family yako.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...