Tarehe 17 Mei: Jumuiya ya WaTanzania nchini Korea Kusini ilipata fursa ya
kutembelea kituo cha Samsung Innovation Museum kujionea teknolojia
mbalimbali zinazotengenezwa na kampuni ya Samsung. Kituo hipo kipo kwenye
campus kubwa ya kampuni ya Samsung Electronics mjini Suwon.
Wanajumuiya WaTanzania nchini Korea wakiongozwa na Mwenyekiti wao
Bwn. Rayton Kwembe (wa pili kushoto) ambaye pia ni mfanyakazi wa Samsung
Electronics Korea wakiingia katika kituo cha Samsung Innovation Museum.
Jumuiya ya WaTanzania wakifuatilia kwa umakini maelezo ya historia ya
teknolojia mbalimbali zilizosaidia kurahisisha maisha.
Wanajumuiya wakifuatilia filamu inayoonyesha jinsi bidhaa mbalimbali za
Samsung zinavyobuniwa kulingana na mahitaji ya binadamu.
Wanajumuiya wakipozi kwa picha nje ya kituo cha Samsung Innovation
Museum baada ya kumaliza ziara. Hakika ilikuwa ni ziara iliyofungua macho.
Mandhari ya
campus kubwa ya
Samsung Electronics mjini
Suwon ambayo ndio
kitovu cha mafanikio ya
Samsung. Campus hiyo ina
jumla ya wafanyakazi
40,000 wanaofanya kazi
kazi idara za masoko na
reseach.
Duh....jumuiya kama familia.....poa sana...wengine hawajaja au kiwanja jiwe????
ReplyDelete