Kamanda Ras Makunja wa Ngoma Africa band ni mwanamuziki mpiganaji aliyepachikwa majina mengi ya utani kutokana na matukio na vibweka vyake.
Unapoutaja muziki wa dansi wa Tanzania maarufu kama "Bongo Dansi" jina la Mwamuziki Ebrahim Makunja aka Kamanda Ras Makunja na mzimu wake wa "Ngoma Africa band" aka FFU-Ughaibuni ama ukipenda waite "Watoto wa Mbwa" au Viumbe wa ajabu "Anunnaki Aliens" yenye makao yake kule Ujerumani, vyote hivyo sawa. 
 Mwanamuziki Kamanda Ras Makunja wa FFU-Ughaibuni, tunamtaja kuwa Mpiganaji na mmoja wa watunzi wachache sana wa muziki  wa dansi ambaye nyimbo au tungo zake zina uzito na ujumbe mkubwa kwa jamii.Maana nyingine nyimbo zake zina mafunzo fulani
Pamoja na sifa hizo mwanamuziki huyu Kamanada Ras Makunja na mzimu wake "Ngoma Africa Band" ukimsikiliza sana utagundua kuwa ujumbe ulio katika nyimbo zake mara nyingine haulezeki rohoni, kwa jinsi unavyolenga au kuzungumzia kero fulani katika jamii
Kwa tabia hizi yeye na bendi yake wamejikuta wakiitwa "Watoto wa Mbwa" yaani wasione kitu lazima watabwaka ! 
Mara nyingine Mtunzi huyu Kamanda Ras Makunja aliyeipindua akili kazi yake,anapoona nyimbo zake zimekuwa cheche za moto huwa anapooza kwa kupeleka ujumbe mzuri kwa jamii wenye kuziteka nyoyo za wengi na kuweza kuzipiga meseji roho za walio wengi "Bongo Tambarare" 
Hapo kamanda Ras Makunja na kikosi chake cha Ngoma Africa Band wanaonekana kuwa watoto wazuri lakini tabia zao ni kama ngozi hazibadiliki wawapo jukwaani ni sawa na askari wa kutuliza ghasia FFU kwa sababu wanajua wazi tabia za washabiki wao za kupenda mdundo live wenye kasi kubwa 
Kwa mtindo huu wamefanikiwa kuteka mamilioni ya washabiki nje na ndani ya ughaibuni. 
Ras Makunja na Muzimu wake "Ngoma Africa Band" wapo ndani ya medani ya muziki wa dansi takribani miaka 21 na kushika chati katika majukwaa ya kimataifa. inasemekana Ngoma Africa band ina himaya yake inayoitwa "Anunnaki Empire" himaya ya viumbe wa ajabu (wasanii na waliowazunguka) katika makao ya bendi,wakiwemo mafundi mitambo ambao kazi yao ni kuhakikisha kila kitu kinacho fanywa ni " Extraordinary" mpaka mziki wenyewe ni "Extraordinary Bongo Dansi". Himaya yao haina uwoga bali inatishia wapinzani wao. 
Mwanamuziki Ras Makunja inasemekana hatumii ulevi wa aina yoyote hile wa kuvuta sigara au ganja, bali ni mtu wa mazoezi makali ya kimwili na kihisia, mazoezi ambayo watu wengi wanadai kuwa yanamsaidia kuongoza kikosi chake anaposafiri na kufanya tour ndefu, pengine katika nchi zenye utamaduni tofauti na wa afrika. 
Kamanda Ras Makunja kufanya nae kazi inabidi uwe mjeshi sio mchezo,kwa sababu hana mdhaa katika kibarua chake. hivi karibuni inasemekana amesharekodi kibao kipya kinachoitwa " Myonge Mnyongeni ! Haki yake Mpeni" wimbo ambao utatolewa baadaye. 
Muziki wa bendi hiyo maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya unasikika pia katika tuvoti at www.ngoma-africa.com pia www.reverbnation.com/ngomaafricaband
Kamanda Ras Makunja wa Ngoma Africa band mwanamuziki mpiganaji
Kamanda Ras Makunja wa Ngoma Africa band (kulia) na kikosi chake

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 26, 2014

    Kamanda mkuu wa kikosi maalumu ughaibuni,field marshal ras makunja
    aka mkuu wa himaya ya viume ajabu anunnaki,kiongozi wa watoto wa mbwa,baba unakubalika nyimbo zenu zina mijiwe mizito

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 26, 2014

    mkulu kulu mungwana kamanda ras makunjas mzee wa kufuga mabundi,naona bado unatisha

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...