Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizawadiwa meza yenye ramani ya Tanzania na Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya rufaa ya Haydom,Dkt.Olav Espegren. Kinana pia alizungumza na Uongozi sambamba na Watumishi wa hospitali hiyo ya Rufaa ya Haydom wilayani Mbulu,mkoani Manyara.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akimshukuru Diwani wa kata ya EShkesh kupitia chama cha CUF,Ndugu Naftari Kitandu alipohudhuria mkutano wa hadhara wa CCM,katika shule ya sekondari ya Yaeda chini,wilayani Mbulu mkoani Manyara.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakaji wa mji wa Mbulu na vitongoji vyake,kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Mbulu,Kinana aliwataka wananchi wa mji huo kuachana na siasa zisizo na tija badala yake wajikite katika miradi mbalimbali ya kujiletea maendeleo na si vinginevy.Katibu Mkuu Ndugu Kinana
ameambatana na Katibu wa NEC Itikad,siasa na Uenezi Nape Nnauye,wakiwa mkoani Manyara kwenye
ziara ya Kukagua kuhimiza na kusukuma miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa
kufuata Ilani ya Chama,kukagua maandalizi ya uchaguzi ya serikali za
mitaa,kusikiliza kero za wananchi na kuzitafututia ufumbuzi.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndug Kinana akiwa amembatana na Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi Nape Nnauye wakiwasalimia wananchi wa mjini Mbulu walipokuwa wakiwasili kwenye mkutano wa hadhara mkoani Manyara.
Sehemu
ya umati wa wakazi wa mji wa mbulu wakishangilia jambo kwenye mkutano
wa hadhara wa CCM,uliofanyika mjini Mbulu mkoani Manyara.
Sehemu
ya umati wa wakazi wa mji wa mbulu wakishangilia jambo kwenye mkutano
wa hadhara wa CCM,wakati Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi,Nape
Nnauye alipokuwa akihutubia mjini Mbulu mkoani Manyara.
Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi,Nape Nnauye akihutubia umati wa watu katika viwanja vya Mbulu mjini,wilayani Mbulu mkoani Manyara.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisaidia kuweka zege kweye renta,ikiwa ni sehemu ya ushiriki wa ujenzi wa jengo la nyumba ya Mwalimu shule ya sekondari ya Yaeda chini Wilayni Mbulu mkoani Manyara.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana (anaendesha mashine ya kushindilia) akishiriki ujenzi na ukaguzi wa daraja la Haydom wilayani Mbulu mkoani Manyara.
Nape Nnauye akishiriki ujenzi wa daraja la Haydom wilayani Mbulu mkoani Manyara.
Huyu Nape anaweza kuja kuwa Rais! Je anaigiza au anafanya kweli?
ReplyDelete