Katibu Mkuu wa CCM,Ndug Kinana akimhoji kwa kifupi Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Hanang, Augustino Mayumba (aliyehudhuria mkutano wa hadhara wa chama cha CCM), alikopeleka hati ya mkataba wa mnara wa simu wa Vodacom uliowekwa katika Kijiji cha Basouto ambao alishiriki kutia saini ambapo hadi sasa malipo ya fedha hizo haijulikani nani analipwa na uko wapi.. 

Hatua hiyo ya kumhoji ilifikiwa baada Kiongozi huyo kuuliza swali kwenye mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika kwenye Kijiji cha Basouto, kuwa viongozi wa CCM wanakula fedha za malipo ya mnara huo uliowekwa eneo la soko. Kinana alimtaka Mayumba aeleze mkataba huo ameuweka wapi. Licha ya kiongozi huyo wa Chadema kukiri kushiriki kusaini mkataba huo lakini alishindwa kueleza kwa kusema kuwa na yeye hajui mkataba huo ulipo, jambo ambalo liliwafanya wananchi kuanza kumzomea. Kinana aliwataka wananchi na serikali kumbana Mayumba hadi aeleze alipouweka mkataba ili serikali ya Kijiji iwe inapata malipo hayo.
Katibu wa NEC Itakadi,Siasa na Uenezi,Nape Nnauye akifurahia jambo na Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Hanang,Bwa.Augustino Mayumba mara baada ya kujibu tuhuma mbele ya Wananchi kwenye mkutano wa hadhara wa CCM,akidaiwa kuficha mkataba wa mnara wa simu wa Vodacom uliowekwa katika Kijiji cha Basouto ambao alishiriki kutia saini ambapo hadi sasa malipo ya fedha hizo haijulikani nani analipwa  na uko wapi.
 Katibu Mkuu wa CCM,akipeana mkono na Katibu Kata wa CHADEMA,wa Kata ya Gendabi,Wilayani Hanang,Bwa,Aman Lucas mara baada ya kukabidhi kadi yake cha chama hicho na kujiunga na chama cha CCM
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa na wafuasi wakuu wa CHADEMA,walioamua kujiunga na chama chama CCM baada ya kuzikabidhi kadi zao kwa Ndugu Kinana.Kulia ni Meshack Kim,Katibu Kata wa CHADEMA,waka Kata ya Gendabi,Wilayani Hanang,Bwa,Aman Lucas na mwisho kushoto ni Elisante Taulo.
Aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Hanang na Waziri Mkuu Mstaafu,Mh.Frederick Sumaye akizungumza jambo na Mbunge wa Jimbo la Hanang, Dk. Mary Nagu walipokuwa kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Gendabi kata ya Gendabi wilayani Hanang mkoani Manyara.
Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi,Nape Nnauye akipokea mabango yenye jumbe mbalimbali yaliokuwa yamebebwa na wananchi,katika mkutano wa hadhara uliofanyika Endasak,Wilayani Hanang mkoani Manyara,pamoja na hayo Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alitoa majibu kwa wananchi hao na kuonesha kuridhika nayo.
 Kinana akuhutubia Wananchi katika Kajiji cha Endasak wilayani Hanang mkoani Manyara.Kinana ameambatana na Katibu wa NEC Itikad,siasa na Uenezi Nape Nnauye,wakiwa kwenye ziara ya Kukagua kuhimiza na kusukuma miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Chama,kukagua maandalizi ya uchaguzi ya serikali za mitaa,kusikiliza kero za wananchi na kuzitafututia ufumbuzi.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya CCM,mjini Katesh,wilayani Hanang mkoani Manyara.Ndugu Kinana ameambatana na Katibu wa NEC Itikad,siasa na Uenezi Nape Nnauye,wakiwa kwenye ziara ya siku saba ya Kukagua kuhimiza na kusukuma miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Chama,kukagua maandalizi ya uchaguzi ya serikali za mitaa,kusikiliza kero za wananchi na kuzitafututia ufumbuzi.
Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi,Nape Nnauye akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya CCM,mjini Katesh,wilayani Hanang mkoani Manyara
Mbunge wa Jimbo la Hanang, Dk. Mary Nagu  akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya CCM,mjini Katesh,wilayani Hanang mkoani Manyara.
Sehemu ya Wananchi wa mjini Katesh wakifuatilia jambo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya CCM,,wilayani Hanang mkoani Manyara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Mwana ukawaMay 28, 2014

    Huu mtandao siku hizi umepoteza mvuto na muelekeo, sivyo kama ulivyoanza!! badala ya kua blog ya jamii kama ilivyokua awali sasa hivi naona imegeuka nakua ni Blog ya CCM!!!, kazi kwelikweli, najua utanibania huu ujumbe wangu sababu nimekuambia ukweli lakini poa, maana siku zote ukweli hua unauma.

    ReplyDelete
  2. sasa wewe mwana ukawa;kwa vile wewe unaichukia ccm ndo habari zake zisiandikwe kwenye blog hii? kwa wengine hizi ni habari kama hujui,kama wewe ni mtambeleaji wa blog hii mara kwa mara unle amejibu sana shutuma zako kama hizo humu kupitia kijiwe cha ughaibuni. Kama wewe inakuuma sana kupublish habari za ccm , ongea na ukawa wamtumiea unle habari zitachapishwa tu bila upendeleo. "yeye(uncle) abagui wala hachagui atakayemzika hamjui"

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 29, 2014

    mjomba hata kama unaichukia CCM lakini uongee ukweli. Mbona kuna wakati tunajaziwa Picha za CHADEMA husemi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...