Katibu MKuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM,Wilaya ya Kaliua,katika ukumbi wa Millenium mkoani Tabora mara baada ya kupokea taarifa mbalimbali za maendeleo ya miradi na hali ya kisiasa wilayani Kaliua. Kinana yupo mkoani Tabora kwa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM, kukagua maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
 Baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Usindi  wakishuhudia Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akikagua mradi wa ujenzi wa jengo la Zahanati ambayo tayari imwekwisha kamilika,isipokuwa inasubiri kibali kutoka Wizara ya Afya na kukamilika nyumba ya mganga.Kinana ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenenezi Nape Nnauye,ambapo walipokelewa na Mbunge wa jimbo la Urambo Magharibi,Mh.Prof Juma Kapuya 
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipata taarifa fupi juu ya mradi wa ujenzi wa jengo la nyumba ya Mganga wilayani Kaliua katika kijiji cha Usindi,Kata ya Ushokora,Katika ziara hiyo ya siku 11,Kinana ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenenezi Nape Nnauye,ambapo walipokelewa na Mbunge wa jimbo la Urambo Magharibi,Mh.Prof Juma Kapuya .
  Katibu Mkuu wa CCM,dugu Kinana  akilakiwa na Mbunge wa jimbo la Urambo Magharibi,Mh.Prof Juma Kapuya,mara baada ya kuwasili wilayani Kaliua,katika kijiji cha Usindi kata ya Ushokora akiwa ameambatana na  Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenenezi Nape Nnauye (hayupo pichani). mkoani Tabora.
Mbunge jimbo la Urambo Mashariki,Mh.Samwel Sitta akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Urambo Magharibi Prof.Juma Kapuya mapema leo kwenye wilaya ya Kaliua,mara baada uusindikiza msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana aliyekuwa Wilayani Urambo Mashariki kwa ziara ya siku 11 ndani ya mkoa wa Tabora.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipokelewa katika kijiji cha Usindi,Kata ya Ushokora wilayani Kaliua mkoani Tabora mapema leo asubuhi,akiwa ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenenezi Nape Nnauye na kupokelewa na Mbunge wa jimbo la Urambo Magharibi,Mh.Prof Juma Kapuya.

PICHA NI MICHUZIJR-KALIUA TABORA
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...