Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana na Msafara wake wakielekea kukagua mradi wa ujenzi wa Daraja la Mto Sibiti linalounganisha wilaya za Meatu mkoani Simiyu na Mkalama, Singida wakati wa ziara yake ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua, kuhimiza na kusukuma ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM, kukagua maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.Kinana leo na viongozi mbalimbali wa chama hicho wakiwemo Mawaziri machachari wataunguruma mjini Singini kwenye mkutano wa hadhara ambao utarushwa LIVE na kituo cha STAR TV
 Mbunge wa Jimbo la Iramba Mashariki, Salome Mwambu akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokwenda kukagua mradi wa ujenzi wa  Daraja la Mto Sibiti linalounganisha wilaya za Meatu mkoani Simiyu na Mkalama, Singida wakati wa ziara yake ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua, kuhimiza na kusukuma ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM, kukagua maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
 Sehemu ya mto wa Sibiti kama uonekavyo pichani
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Parseko Kone (kulia), wakitoka kukagua ujenzi wa Daraja la Mto Sibiti linalounganisha wilaya za Meatu mkoani Simiyu na Mkalama, Singida wakati wa ziara yake ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua, kuhimiza na kusukuma ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM, kukagua maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi,Nape Nnauye akiwahutubia wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Gumanga,Kata ya Gumanga, wilayani Mkalama mkoani Singida.
 Kinana akisoma majina ya vijiji lukuki vitakavyopata umeme katika Wilaya mpya ya Mkalama, Kata ya Nduguti,Jimbo la Iramba Mashariki, mkoani Singida.
 Kinana akiwapungia Wananchi waliokuwa wamekusanyika kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Wilaya mpya ya Mkalama, Kata ya Nduguti,Jimbo la Iramba Mashariki, mkoani Singida.Pichani kati ni Katibu wa NEC Itikadi Siasa na Uenezi,Nape Nnauye pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Mwigulu Nchemba
Wananchi wakiwa wamekusanyika kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Wilaya mpya ya Mkalama, Kata ya Nduguti,Jimbo la Iramba Mashariki, mkoani Singida.ambapo katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana aliwahutubia.

PICHA NA MICHUZIJR-MKALAMA SINGIDA
PICHA ZAIDI BOFYA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...