Mkuu wa idara ya utalii katika hifadhi ya taifa ya mlima Kilimanjaro Eva Mallya akitoa ufafanuzi juu ya utaratibu mpya wa kuhamasisha utalii wa ndani.kushoto kwake ni afisa Masoko wa hifadhi hiyo Antipas
Juu na chini ni baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza kwa umakini mkuu wa idara ya utalii katika hifadhi ya mlima Kilimanjaro Eva Mallya 
Na Dixon Busagaga wa Globu 
ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

HIFADHI ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro ,imetoa fursa kwa wananchi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa jumla kupanda mlima Kilimanjaro hadi kilele cha Shira (Shira Plateu) kwa nusu bei yaani shilingi 5,000 kwa watu wazima kuanzia miaka 16 na kuendelea na Shilingi 1,000 kwa watoto kuanzia miaka 5 hadi 15.
Gharama hii ni nusu ya bei halisi ambayo ni shilingi 10,000 kwa watu wazima na 2,000 kwa watoto.Ofa hii inaanza Mei 15 hadi Mei 18 mwaka huu,Safari hiyo itakuwa ya kutwa nzima kwenda na kurudi siku hiyo hiyo na usafiri utatolewa bure na hifadhi (KINAPA).
Vituo vya kujiandikishia ni mgahawa wa Fresh coach Moshi mjini ,Hosptal ya KCMC,Njia Panda ya Himo (Stand ya Same),Bomang’ombe (Kiwire Supermarket) na KINAPA Marangu(Mapokezi).Kazi ya uandikishaji imeanza tayari.Vituo vitakuwa wazi kuanzia saa 2 asubuhi.Wanaopenda kupanda wanashauriwa kufika katika maeneo hayo tajwa.
Vituo vya kuanzia safari ni viwili Mgahawa wa Fresh Coach Moshi mjini na Bomang’ombe (Kiwire Supermarket),Safari itaanza saa moja kamili asubuhi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 13, 2014

    Nadhani ni mpango mzuri japo ungehitaji kuongeza muda angalau wa Juma moja. Pia usajili kwa Watu walio mbali ungefanywa kwa Njia ya Ki-electroniki na malipo kadharika ili kuongeza idadi ya watalii wa ndani

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...