Mkutano
Mkuu wa 9 Ngazi ya Mawaziri katika Shirika la Biashara la Dunia “World Trade Organization (WTO)”
uliofanyika kutoka tarehe 3 hadi 6 Desemba, 2013 katika mji wa Bali, Indonesia
uliazimia kuboresha taratibu za kiforodha ili zifanyike kwa haraka na ufanisi
mkubwa kuliko ilivyo ilivyo sasa kupitia ushirikiano kati ya mamlaka za forodha
za nchi wanachama.
Makubaliano
hayo pia yamechukua mahitaji ya Nchi zinazoendelea na zile zilizo changa kama
vile Tanzania kwa kubeba misimamo ya msaada wa Kiufundi na kujenga uwezo katika
Uwezeshaji Biashara.
Kwa
kutambua fursa zilizo ndani ya Makubaliano ya Uwezeshaji Biashara na changamoto
zinazozikabili Nchi changa katika utekelezaji wa makubaliano hayo, Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia
Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kushirikiana na “East African Research Capacity Development Foundation (EARCDF)”,
“Nordic Africa Institute (NAI) of Sweden” na “SITRADE” imeandaa Kongamano la siku 3 ambalo linafahamika kama
“kongamano
la uwezeshaji biashara baada ya mkutano mkuu wa bali kwa nchi changa za afrika
kuanzia tarehe 14 mpaka 16 Mei, 2014 katika Hoteli ya Snow Gold Crest Mwanza,
Tanzania.
Kongamano
hili litahudhuriwa na Vionngozi na Maafisa wa Wizara ya Viwanda na Biashara
Tanzania, Mabalozi Modest J. Mero
(Ubalozi wa Kudumu Tanzania, Geneva) ambaye kwa sasa ni Msemaji (Negotiator) na
Mratibu katika maswala ya Uwezeshaji Biashara katika Shirika la Biashara la
Dunia (WTO) kwa niaba ya Nchi Changa; na Balozi Ali Mchumo (Aliyekuwa
Mwenyekiti wa Baraza Kuu la WTO).
Pia
watakuwepo Wajumbe 22 wa Nchi changa za Afrika ambazo ni mwanachama wa Shirika
la WTO. Washiriki wengine watakuwa takribani 40 ambapo idadi yao inajumuisha
wataalam waliobobea katika maswala mbalimbali, wakiwemo watafiti wa maswala ya
Biashara na mameneja wa Sera za Biashara kutoka katika ngazi za juu.
Kongamano
hili linalenga kuakisi Agenda ya
Uwezeshaji Biashara baada ya Bali ambapo ndani yake kuna masuala muhimu na
mpango kazi kwa Nchi Changa za Afrika. Dhima hii inalenga maeneo muhimu
ambayo ni:
i.
Uelewa katika mtazamo wa
kihistoria, dhana, msingi na hatua mbalimbali ambazo dhana ya Uwezeshaji
Biashara imepitia
ii.
Hali ya muonekano wa Uwezeshaji
Biashara katika Jumuiya za Uchumi Kikanda Afrika “Trade Facilitation in African
Regional Economic Communities (RECs)”;
iii. Kutumia
uzoefu utakaokuwa umepatikana ili kutengeneza mapendekezo ya agenda kazi ya
utekelezaji wa makubaliano ya WTO katika Uwezeshaji Biashara.
Imetolewa
na,
WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA
DAR ES SALAAM
MEI 12, 2014.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...