Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo, kwa niaba yaya Waziri wa
Viwanda na Biashara Mhe. Dkt Abdallah Kigoda, akifungua Kongamano la uwezeshaji
biashara baada ya mkutano mkuu wa Bali kwa nchi changa linalofanyika Mkoani
Mwanza, Mei 16 hadi 16, 2014.
Meza kuu katika Kongamano hilo.
Viongozi Wakuu katika Kongamano hilo, Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya
Mtangamano wa Biashara Bw Lucas Saronga, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi
Evarist Ndikilo, Profesa Francis Matambalya , Balozi Mstaafu Ali Mchumo na Balozi wa
Tanzania- Umoja wa Matafaifa Bw Modest Mero.
Picha ya Pamoja ya Wajumbe na Viongozi wakuu wa Kongamano la uwezeshaji
biashara baada ya mkutano mkuu wa Bali kwa nchi changa linalofanyika Mkoani
Mwanza, Mei 16 hadi 16, 2014.
Serikali imerudia wito wake kwa sekta binafsi na Wadau wa Maendeleo kuunganisha
nguvu zao katika kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara nchini na kutumia vyema
fursa za kitaifa na kimataifa ili kuinufaisha nchi na wananchi kwa ujumla.
Wito huo umetolewa na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt Abdallah Kigoda
katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi
Evarist Ndikilo katika Ufunguzi wa kongamano la uwezeshaji biashara baada ya
mkutano mkuu wa Bali kwa nchi changa za Afrika.
Waziri Kigoda amesema, Serikali itaendelea kusimamia juhudi zake katika kupunguza
gharama za kufanya biashara na kuondoa vikwazo vya kibiashara ili kufanya shughuli
hizo kufanyika kwa wepesi, muda mfupi, ufanisi na tija kwa wadau wote.
Amesisitiza kuwa, wakati nchi ikifanya juhudi hizo, ni wakati muafaka sasa kwa nchi
zilizoendelea kutimiza makubaliano yaliyofikiwa katika Mkutano wa Bali mwaka 2013
ambapo nchi hizo zilipewa wajibu wa kuzisaidia nchi masiki kifedha, miundo mbinu na
teknolojia ili kuzisaidia nchi masikini kupiga hatua.
Kwa upande wake Kiongozi wa Waandaaji wa Mkutano huo Profesa Francis
Matambalya amesema, Kongamano hili ni fursa muafaka ya kupokea mawazo na
uzoefu wa nchi washiriki ili kutoka na msimamo wa pamoja wa kiutekelezaji kuhusu
maazimio ya Mkutano wa Bali.
Maeneo yanayopewa umuhimu mkubwa na Kongamano hili ni kukuza uelewa
katika mtazamo wa kihistoria, dhana, msingi na hatua mbalimbali ambazo dhana ya
Uwezeshaji Biashara imepitia, Hali ya muonekano wa Uwezeshaji Biashara katika
Jumuiya za Uchumi Kikanda Afrika na namna bora ya kutumia uzoefu utakaopatikana
ili kutengeneza mapendekezo ya agenda kazi ya utekelezaji wa makubaliano ya WTO
katika Uwezeshaji Biashara.
Kongamano hili la siku mbili linahudhuriwa na Mabalozi, Viongozi wa Wizara ya
Viwanda na Biashara, washiriki kutoka nchi zaidi ya kumi na saba kutoka nchi change
za Kiafrika na Wawakilishi wa Taasisi mbali mbali za kitaifa na Kimataifa.
Kongamano lingine hilo!!!
ReplyDelete