Tamasha kubwa la watoto ‘Extreme Kids Festival’ litakalofanyika May 31 na June 1 katika viwanja vya Leaders Club, Dar es Salaam na litapambwa na mwimbaji mkongwe wa kike anaependwa sana, Lady Jay Dee.

Lady Jay Dee atajumuika na watoto watakaohudhuria tamasha hilo, atawaongoza kuimba nyimbo mbalimbali ili kuwahamasisha kuonesha vipaji vyao na atawapa zawadi wale watakaofanya vizuri zaidi.

“Watoto Mambo vipi, Jay Dee nawakaribisha watoto wote pamoja na wazazi na walezi. Mje basi katika Extreme Kids Festival. Ni Jumamosi ya tarehe 31 May, si hapo tu na Jumapili ya tarehe 1 June. Tunatoa nafasi kwa watoto kuzindua vipaji vyao vya kuimba na washindi watapata zawadi.” Amesema Lady Jay Dee kwenye maelezo yake.

Katika tamasha hilo, mbali na michezo/games mbalimbali inayopendwa zaidi na watoto pia kutakuwa na semina fupi kwa ajili ya wazazi na walezi kwa ajili ya kuboresha malezi ya watoto.

Kutakuwa pia na bidhaa mbalimbali huduma muhimu bora zaidi kwa ajili ya watoto na wanafamilia zitatolewa kwa siku hizo mbili. Waandaaji wa Extreme Kids Festival wamesisitiza kuwa kutakuwa na usalama wa kutosha kwa ajili ya watoto na wote watakaohudhuria na kwamba hakutakuwa na pombe .

Watoto watalipa shilingi 3,000 tu na wakubwa watalipa shilingi 5, 000 tu kuingia katika tamasha hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...