Miaka ya nyuma ilikuwa Tajiri mwenye Basi akitaka kuajiri Dereva Swali la Msingi iliuweze kuajiariwa alikuwa anauliza kama Umewahi kuendesha wapi na wapi Ukitaja UDA kazi unapata haraka sana Tofauti na sasahivi madereva wa uda wamekuwa hawana sifa kwani tunashudia wanavyo endesha hovyo magari hayo Barabarani na hawaheshimu kabisa taratibu za uendeshaji.Ni jana usiku tu tumeona moja ya gari hilo likiwa mtaroni kutokana na uzembe wa madereva hao,sasa na asubuhi ya leo tunaona basi lingine likiwa na tatizo hilo hilo huku wahusika wakiingia mitini.Je kuna nini kinaendelea nyuma ya pazia???.Picha na Mdau Chriss Mfinanga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 24, 2014

    kuna UDA number 048 sitalisahau jamaa anaendesha ovyo sana alinipiga pini roun about ya askari wakati yy alikuwa nyuma yangu akani overtake kwa kutumia mabavu ikabidi nipaki pembeni kumpisha....awa madereva wataua magari yote yale....lkn hii ni ishara ya uongozi mbovu we unampaje UDA dereva humuwapimi kilevi on daily or weekly basis? au kujua historia yao?

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 24, 2014

    Yaani UDA ni tatizo afu wanajiamini kupita kiasi, namshukuru Mdau aliyelileta hili hapa mezani, naomba uwekwe mjadala maalum kuhusu UDA, watatumaliza

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 25, 2014

    Jambo jingine mabasi yao yapewe root maalumu kwani yanatupa shida hayajulikani yanakoelekea mpaka uulize. Nashauri yaandikwe kama ilivyo kwa daladala nyingine.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 25, 2014

    Tatizo la UDA ni kubwa na linaanzia juu kabisa. Lakini kama Mh. Spika amelizima bungeni, ninyi mtaongelea nini. ...na samaki uoza kuanzia kichwani!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...