Na John Gagarini, Kibaha
JESHI la Polisi mkoani Pwani linamshikilia dereva Frank Chabayanga
(39) mkazi wa Morogoro wa basi la kampuni ya BM kwa tuhuma za kumgonga
mtembea kwa miguu na kusababisha kifo chake.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoani Pwani Kamishna Msaidizi
Mwandamizi (SACP) Ulrich Matei (pichani) amesema kuwa tukio hilo limetokea Mei
20 mwaka huu majira ya saa 3:30 Usiku eneo la Kwa Mbonde wilayani
Kibaha katika barabara kuu ya Dar es Salaam Morogoro.
Kamanda Matei amesema kuwa mtuhumiwa alikuwa akiendesha gari aina ya
Yu Tong lenye namba za usajili T 919 CAB alimgonga mtu ambaye jina
lake halikuweza kutambuliwa mara moja.
Aidha alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo wa kasi ambapo
mwili wa marehemu umehifadhiwa kwnye hospitali ya Rufaa ya Tumbi.
Kwenye tukio lingine dereva Issa Kidito (64) mkazi wa Dar es salaam anashikiliwa
kwa tuhuma za kumgonga mpanda baiskeli na kusababisha kifo.
Kamanda Matei amesema kuwa mtuhumiwa alikuwa akiendesha gari aina ya
Toyota Land Cruiser hard top lenye namba za usajili namba T 722 ABA
aliwagonga wapanda baiskeli na kusababisha kifo cha Mwalimu Hamisi
Mtanga (58).
Amebainisha kuwa tukio hilo lilitokea kitongoji cha Londondo Kijiji
cha Kiwanga Kata ya Chumbi tarafa ya Muhoro wilaya ya Rufiji ambapo
mtuhumiwa huyo alikuwa akielekea mkoani Lindi aliacha barabara na
kumgonga mwendesha baiskeli huyo ambaye ni mwalimu wa shule ya msingi
Mihilu na kufariki papo hapo huku abiria wake Mussa Ndolela
akijeruhiwa na kulazwa kituo cha afya Muhoro.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...