Mnamo tarehe 28 Aprili 2014 Mheshimiwa Mzee Kenneth David Kaunda (KK), Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Zambia alifikisha miaka tisini (90). Sherehe kubwa iliandaliwa siku hiyo ambapo Mama Maria Nyerere alialikwa lakini kwa sababu zisizozuilika hakuweza kuhudhuria. Ili kukamilisha nia hiyo Mama Nyerere akamtuma mwanae Mheshimiwa Makongoro Nyerere ambae pia ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki kuja kuwasilisha salamu za pongezi zake binafsi na za familia ya Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Baba wa Taifa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Makongoro pamoja na salamu alimkabidhi Mheshimiwa Mzee Kaunda zawadi ya kinyago ambacho kilitafsiriwa kama Umoja na Mshikamano. Katika hafla hiyo aliongozana na Balozi wa Tanzania nchini Zambia Mheshimiwa Grace Mujuma.

Baada ya kupokea salaam na kinyago Mzee Kaunda alitoa shukrani zake nyingi kwa familia ya Hayati Baba wa Taifa kwa kumkumbuka na kusherehekea naye kufikia umri huo.
Mzee Kenneth David Kaunda (KK) akipokea zawadi aliyotunukiwa na Mama Maria Nyerere. Anaye mkabidhi zawadi hiyo ni motto wake Mhe. Makongoro Nyerere akishuhudiwa na Mhe. Balozi Grace Mujuma.
Mzee KK akiwa na zawadi yake ya Kinyago alichotunukiwa na Mama Maria Nyerere.
Mzee Kaunda akiwa kwenye picha ya pamoja na binti yake Catherine Kaunda, Mhe Makongoro Nyerere na Mhe Balozi Grace Mujuma.
Mhe. Makongoro Nyerere akiweka saini kitabu cha wageni katika Ofisi ya Mhe. Balozi Grace Mujuma akishuhudiwa na Afisa wa Ubalozi huo Bw. Richard Lupembe.
Mhe Makongoro Nyerere akiwa katika picha ya pamoja na Mhe Balozi Grace Mujuma pamoja na Afisa wa Ubalozi Bw. Richard Lupembe kwenye Ofisi za Ubalozi wa Tanzania Lusaka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...