Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) Dk. Reginald Mengi (wa tatu kulia) akikata utepe kuzinduwa maonesho ya biashara ya bidhaa kutoka nchi za Uturuki na Tanzania leo jijini Dar es Salaam yanayofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee kuanzia leo tarehe 15 hadi tarehe 17, 2014.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) Dk. Reginald Mengi, ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, akizungumza na wafanyabiashara wanaoshiriki maonesho ya biashara ya bidhaa kutoka nchi za Uturuki na Tanzania kabla ya kuyafungua rasmi maonesho hayo leo jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo yameanza leo tarehe 15 hadi tarehe 17, 2014.
Bidhaa ya wananchi wakiangalia bidhaa mbalimbali kutoka zinazooneshwa katika Maonesho ya Biashara ya bidhaa kutoka nchi za Uturuki na Tanzania yanayofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Bidhaa mbalimbali kutoka Tanzania zikioneshwa katika Maonesho ya Biashara ya bidhaa kutoka nchi za Uturuki na Tanzania.

Hivi ni "Maonesho" au "Maonyesho"?
ReplyDeletekiswahili sanifu ni "maonesho"
Delete