Jamii ya Mara Group ya Mji mdogo wa Mererani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, imemchagua Philemon Oboro, kuwa Mwenyekiti wake kwa kipindi cha miaka mitatu baada ya kuwaangusha wapinzani wake watatu.
Akitangaza matokeo hayo jana, Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi huo Samwel Ombeng alisema Oboro alipata kura 523, Philipo Mtanda Onyando kura 60, Allan Gichana kura 33 na Jackson Onyango Mutaban kura nane.
Ombeng alisema Elija Ambonya alichaguliwa kuwa Mwenyekiti Msaidizi kwa kupata kura 363 na kumshinda Thobias Magati aliyepata kura 305 na Stephen Odoya, alichaguliwa kuwa Mweka hazina, baada ya kukosa mpinzani.
Naye, katibu wa tume hiyo Gerald Orinya alisema Elija Ambonya alichaguliwa kuwa Katibu wa Mara Group kwa kupata kura 363 na kuwashinda Adam Wambura kura 117, Msafiri Marwa kura 130 na Omenda Odero kura 84.
Orinya alisema George Okwaro alishinda nafasi ya Katibu msaidizi kwa kupata kura 378 na kumshinda Samwel Orafa aliyepata kura 221 na Asubuhi Kibaso alishinda nafasi ya Kamanda wa Mara Group, baada ya kupita bila kupingwa.
Katibu wa Utegi kaskazini, Atanas Ongati (Power Tiler) alisema lengo la Mara Group ni kusaidiana kwenye shida na raha na kuhakikisha watu wote wanaofariki wakiwa Mirerani wanasafirishwa na kwenda kuzikwa nyumbani kwao mkoani Mara.
Akizungumza baada ya kuchaguliwa, Oboro alisema atawaongoza ipasavyo wana kikundi hao bila ubaguzi na dhamira yake ni kuwaunganisha pamoja kwa kutojali waliompigia kura au wasiompigia kwani wote ni wamoja.
Naye, Mwenyekiti msaidizi Ambonya alisema kupitia ushirikiano walionao watahakikisha Mara Group inazidi kuimarika na kusaidiana na jamii yote ya mji mdogo wa Mirerani bila kujali tofauti, kwani ushirikiano ndiyo nguzo ya umoja.
Jamii ya Mara Group ya Mji mdogo wa Mererani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wakiwa wamembeba Mwenyekiti wao, Philemon Oboro aliyechaguliwa jana kwa kupata kura 523 hivyo kuongoza jamii hiyo kwa muda wa miaka mitatu.
Jamii ya Mara Group ya Mji mdogo wa Mererani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wakiwa wamembeba Makamu Mwenyekiti wao, Elija Ambonya aliyechaguliwa jana kwa kupata kura 363 hivyo kuongoza jamii hiyo kwa muda wa miaka mitatu.
Mara Group pongezi kwa kupata Kiongozi mpya na pia sasa muache kuvuta(bangi) na kunywa(gongo) badala yake mfanye kazi kwa bidii kuwa Raia wema na kutii amri za POLISI na SERIKALI!
ReplyDeleteNdugu zetu wa Mkoa wa Mara ni Wachapa kazi lakini ni wakorofi kupita maelezo!
ReplyDeleteHebu tazameni hiyo hoya hoya hapo tu,ilekupmata Raisi wenu wa Mara mpya mchaka mchaka kiasi cha kuashiria uvunjifu wa amani!!!
Mara ndugu zetu mna fujo sana!
ReplyDeleteNdio maana mmewekewa Polisi za Kanda za Mikoa hadi Vijijini!!!
Mkivunja amani Tanzania kama dalili za hayo mnayofanya hapo haitakuwa tabu sana kwakuwa tunayo Afrika ya Mashariki, tutawahamishia Kenya!
ReplyDeleteMimi ni Mtani wenu Mzaramo wa Darisalama nitakuja na Ngariba kuanza kazi rasmi nitamwambia Ngariba aanzie kwa Mwenyekiti mliye mchagua na kuendelea zaidi kwenye kundi lote hilo kutoka kwa mmoja hadi mwingine !
ReplyDelete