Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera ( kulia) akionesha kitu wakati Meneja wa Tanrords Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Dorothy Mtenga ( kushoto ) akiangalia eneo la maji lililijaa katika mto Kilombero mei 5, mwaka huu, wakati Mkuu huyo wa Mkoa na kamati yake ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa ilipotembelea eneo la Kivukoni kuona madhara ya mafuriko.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, akiwa ndani ya boti kwenye mto Kilombero , mei 5, mwaka huu ,tayari kuanza safari ya kurejea eneo sehemu ya kituo cha kupandia abiria umbali wa kilometa zipatazo 1.5.
eneo la ujenzi wa tuta la barabara ya kuingilia kwenye Kivuko cha Kilombero ambayo imebomolewa na maji ya mafuriko ya mvua na kusababisha magari kushindwa kupita eneo hilo ambalo lina urefu wa mita 65 na kipande kikubwa kubwa ni mita 30 kama walivyokutwa Mei 5, 2014 eneo hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...