Na Mwandishi
Wetu, Dar es Salaam
MWIMBAJI wa
muziki wa kizazi kipya, Mbwana Mohamed Mb Dog, amesema baada ya kuachia video
yake ya ‘Mbona Umenuna’, anaendelea na juhudi za kuwapatia raha wadau na
mashabiki wake kama njia ya kuonyesha makali yake kisanaa.
Akizungumza
jana jijini Dar es Salaam, Mb Dog alisema video yake imeandaliwa kwa kiwango
cha juu, huku ikiwa ni sababu ya yeye kuendelea kutoa nyimbo nzuri
zinazoonyesha ubora wake.
Alisema kuwa
lengo lake ni kufanya makubwa zaidi katika tasnia ya muziki wa Bongo Fleva,
hasa baada ya kuamua kurudi tena katika soko hilo kwa mikakati ya aina yake.
“Nipo katika
harakati za kuonyesha namna gani naweza kuonyesha ubora wangu kama ilivyokuwa
mwanzo nilipotoka na wimbo wa kwanza wa Latifa, nikiwa na ‘Madee’.
“Naamini hii
ni njia nzuri ya kuwapatia burudani kamili wadau na mashabiki wangu katika
tasnia ya muziki wa kizazi kipya, hasa baada ya kuachia video yangu ya Mbona
Umenuna,” alisema Mb Dog.
Mb Dog yupo
kwenye harakati kabambe ya kumrudisha kileleni kwenye sanaa ya Bongo Fleva,
akitokea chini ya Kampuni ya Qs Mhonda J Entertainment, yenye maskani yake
jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...