Mkaguzi kutoka Sumatra akiongea na Vyombo vya habari na madereva na makondakta
 Kamanda wa Polisi kinondoni akitoa mrejesho kwa waandishi wa habari baada ya kuweza kukubaliana na Madereva na Makondakta kutumia barabara kuu kwa siku mbili ili wakati wakiendelea kushughulikia utaratibu wa kutengenezwa kwa barabara za ndani ambazo walikuwa wanapaswa kuzitumia

 Abiria wanaotumia njia ya makumbusho kuelekea Mwenge wakitokea Tandika na Mbagala jijini Dar es salaam leo wameonja Joto ya jiwe kwa takribani masaa manne baada ya mabasi yanayotumia kituo cha ndani kugoma kupeleka abiria Mwenge kutokana na ubovu wa barabara za ndani wanazotumia kupita kuelekea kituo hicho. 
Sakata hilo lilianza pale magari yalipofika kituo cha ndani cha Makumbusho na kuwashusha abiria wote na kugoma kuendelea na safari ya kuelekea mwenge,ndipo mzozo mkubwa ulipozuka na kupelekea Sumatra na vyombo vya Usalama kufika eneo La Tukio na kuweza kuongea na madereva hao,lakini madereva hao na makondakta waliendelea kugoma mpaka pale walipohaidiwa kuwa ndani ya wiki moja barabara hizo zitakuwa zimerekebishwa na kuwa nzuri,hivyo watumie njia kuu kuelekea mwenge.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 27, 2014

    Ni dalili ya kuanza kutambua haki zao za msingi.....kila kundi litakuja kutambua haki zao kwa wakati wao.....alafu itaonekana kama vile tumechelewa!!!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 27, 2014

    Haki gani? Kuvunja sheria za nchi ndio kutambua haki? Wewe Mdau acha kuposha umma. Nakubali kuna matatizo na changamoto lukuki kwenye uongozi wetu lakini suluhuhisho si kuleta vurugu na usumbufu kwa jamii ili mradi eti mnajua haki yenu. Watu watoe hoja za msingi na kuwabana viongozi ili walete suluhisho badala uvunjifu wa amani.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 27, 2014

    Eeh! Tunaomba Serikali irudishe barabara za Kijitonyama na Makumbusho kama zilivyokuwa JAMANI zimekuwa na maandaki makubwa. Haiwezekani m-direct daladala zote ziingie ndani na kusababisha barabara zote za maeneo hayo kuaribika wakisha goma ndio mnazitelekeza. Kinachotuumiza zaidi ni ile barabara ya Akachube iliyijengwa kwa ROAD FUND ambayo sijui ilikuwa ya majaribio au lah! Hata mwaka mmoja haikufikisha iko kama ya mwaka 1947!!! Mtujengee barabara zetu, na hayo madaladala mtuondolee.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...