Mh.Saada M.Salum akifafanua jambo katika moja ya Mikutano ya Magavana wa
Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na watendaji wa mashirika mbalimbali
ya Kimataifa,Kulia kwa Mh.Waziri ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha – Dkt.
Servacius Likwelile na Kushoto ni Bwa.Peter Noni Mkurugenzi Mkuu wa Benki
ya Rasimali Tanzania (TIB).
Mh.Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum na Washiriki mbalimbali wa Mkutano
wa mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika mara baada ya ufunguzi wa Mkutano
huo uliofunguliwa na Mh.Paul Kagame katika ukumbi wa Mount Karisimbi Jijini
Kigali Rwanda.
Serikali ya Tanzania ipo imara katika kuendelea na kusimamia juhudi zinazofanywa na Banki ya
Afrika katika kuinua mitaji kupitia mpango wa sita wa kukuza mitaji wa benki hiyo (GCI-VI).
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum alipokuwa akitoa hotuba yake
kwa Magavana wa nchi za Afrika katika mkutano wa mwaka wa wadau wa Benki ya Afrika
jijini Kigali, Rwanda.
Mh.Saada amesema kuwa kupitia mpango wa GCI-VI Tanzania imekuwa na uwezo wa
kulipa hisa zake zipatazo Dola za Kimarekani 2,683,429.52 katika awamu ya tatu kwa muda
uliopangwa.
Saada amesema kuwa kupitia mpango wa GCI-VI Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika
kulipa hisa zake zipatazo Dola za Kimarekani 2,683,429.52 katika awamu ya tatu kwa muda
uliopangwa.
Zaidi ya hayo, Waziri Saada ameendelea kusema kuwa nchi yake imeweza kulipa hisa zake za
awamu ya nne zipatazo kiasi cha Dola za Kimareka 1,279.30 kabala ya muda uliopangwa.
“Ninaamini ni katika mkutano huu tunaweza kujadili dira ya Benki katika miaka mingine 50
ijayo kama kauli mbiu ya mkutano huu inavyothibitisha, “Afrika tunayoitaka miaka 50 ijayo”
alisema Waziri Saada.
Aidha, Waziri Saada alimpongeza Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Dkt. Donald
Kaberuka na uongozi mzima kwa kusimamia na kuongoza kwa umahiri mkubwa majukumu
walionayo ya kibenki na kuhakikisha inasonga mbele daima na kuifanya kuwa benki bora barani
humu.
Ili kuhakikisha malengo hayo yanafikiwa bara hili lazima kudumisha ushirikiano katika Nyanja
mbalimbali za kijamii na kujipatia maendeleo endelevu kwa nchi zao na watu wake. Mwaka huu
Benki ya Afrika inafikisha miaka 50 tangu kuasisiwa kwake ambapo imeendelea kuhudumia
bara hili kwa mafanikio makubwa.
Kwa upande wake Rais wa Rwanda Paul Kagame akifungua mkutano huo alisema kuwa
ili kufikia uchumi wa kati katika Bara la Afrika kwa miaka 50 ijayo inabidi nguvu kubwa
ielekezwe kwenye sekta binafsi ambayo itatengeneza ajira kwa vijana na wanawake.
Mkutano huo ni wa siku tano kuanzia 19 hadi 23 Mei mwaka huu ambapo kabla ya ufunguzi wa
Mkutano huu ulitanguliwa na mikutano mbalimbali ya Magavana ambao ni Mawaziri wa Fedha
kutoka nchi mbalimbali barani Afrika wakiambatana na wajumbe kuwakilisha nchi zao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...