Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni Bw. Celestine Onditi wa pili kulia ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mkutano wa Wadau wa Ukusanyaji Maoni Sheria ya Uongezaji Thamani Madini akiwa katika picha ya pamoja na wadau hao. Wa kwanza kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Sheria ya Uongezaji Thamani Madini , Mhandisi Hamis Komba, ( wa tatu kushoto) ni Kamishna Msaidizi wa Uchumi na Biashara Mhandisi Salim Salim, Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kusini Mhandisi Benjamin Mchwampaka wa kwanza kulia ni Kamishna Msaidizi wa Kanda Magharibi Shubi Byabato.
Baadhi ya Wadau wa Sheria ya Uongezaji Thamani Madini wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa wakati wa mkutano huo.
Katibu Tawala wa Wilaya Kinondoni Bw. Celestine Onditi akisalimiana na baadhi ya wadau wa Sheria ya Uongezaji Thamani Madini mara baada ya kufungua mkutano huo. Katikati ni Kamishna Msaidizi wa Sheria ya Uongezaji Thamani Madini, Mhandisi Hamis Komba.
Mhandisi Madini na Uchenjuaji Migodi Wizara ya Nishati na Madini Asnath Mkani akiwasilisha mada ya Historia ya Uongezaji Thamani Madini nchini.
Na Asteria Muhozya, Dare s Salaam
Katika picha ni mkutano wa wadau wa Sheria ya Uongezaji Thamani Madini
unaoendelea jijini Dar es Salaam baada ya mkutano kama huo uliofanyika
mwishoni mwa wiki Jijini Arusha. Mikutano hiyo inafanyika ili kupata maoni ya
wadau wa tasnia ya madini ya vito na usonara kwa ajili ya Rasimu ya Sheria hiyo .
Wakati akifungua mkutano huo jana, Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni Bw.
Celestine Onditi aliwataka wadau kutoa maoni yao ili iweze kupatikana Sheria
ambayo itakuwa ni shirikishi akiunganisha maoni ya wadau wote wa sekta ya
madini hali itakayosaidia . Ameongeza endapo wadau watatoa maoni stahiki
Sheria hiyo itasaidia sekta ya madini kuchangia kwa pato la Serikali kwa kiasi
kikubwa zaidi ikizingatia kuwa, nchi ya tanzania imebarikiwa kuwa na hazina
kubwa ya madini ya aina mbalimbali.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Magesa Mulongo wakati
akifungua mkutano kama huo jijini Arusha aliwataka wadau wa Sheria kutoa
maoni yatakayosaidia Sheria hiyo kuwa yenye tija kwa manufaa ya taifa na
watanzania.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...