Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara Bw. Salum Masalanga (katikati) akikabidhi msaada wa pedi kwa Mwanafunzi wa Shule ya Msingi ya Maendeleo, Neema Mohamed chini ya programu ya Hakuna Wasichoweza iliyofadhiliwa na Vodacom na T-MARC. Wakishuhudia tukio hilo, ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii Vodacom, Yesaya Mwakifulefule (kushoto)na Mratibu wa Mradi kutoka T-MARC Tanzania, Bi. Dorice Chalambo (kulia), mradi huo umeanza kufanya kazi mkoa wa Mtwara na Lindi na kusambaa nchi nzima.
Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara Bw. Salumu Masalanga (katikati) akipokea msaada wa pedi kwa niaba ya wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Maendeleo chini ya programu ya Hakuna Wasichoweza iliyofadhiliwa na Vodacom na T-MARC. Wakishuhudia tukio hilo, ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii Vodacom, Yesaya Mwakifulefule (kushoto) na Mratibu wa Mradi kutoka T-MARC Tanzania, Bi. Dorice Chalambo (wa pili kulia), mradi huo umeanza kufanya kazi mkoa wa Mtwara na Lindi na kusambaa nchi nzima.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii Vodacom, Yesaya Mwakifulefule (kushoto) na Mratibu wa Mradi kutoka T-MARC Tanzania, Bi. Dorice Chalambo (wa pili kulia) kwa pamoja wakikabidhi msaada wa pedi kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Maendeleo chini ya programu ya Hakuna Wasichoweza iliyofadhiliwa na Vodacom na T-MARC. Akishuhudia tukio hilo (katikati) ni Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara Bw. Salumu Masalanga, mradi huo umeanza kufanya kazi mkoa wa Mtwara na Lindi na kusambaa nchi nzima.

Wasichana wa mkoani Mtwara wamefaidika na elimu ya afya pamoja na vifaa vitakavyowasaidia kujisitiri wakati wa hedhi. Elimu hii na msaada vimetolewa kupitia mradi wa Hakuna Wasichoweza unaotekelezwa na asasi ya T-MARC Tanzania. 

Mradi wa Hakuna Wasichoweza unaendeshwa na asasi ya T-MARC Tanzania kwa ufadhili wa watu wa Marekani kupitia Shirika la Maendeleo la Kimarekani USAID kwa ushirikiano na Vodacom Foundation.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 01, 2014

    Hiki kichwa cha habari kinashtua! labda ingenukuliwa "...vifaa vya kujisitiri kwa wasichana".

    ReplyDelete
  2. Tujenge vyoo vya kisasa mashuleni na kuhakikisha uwepo wa Maji safi daima. Ugawaji wa vifaa vya msimu siyo endelevu. Tuwafunze wasichana kushona na kutumia zana asilia. Tulishona, tukatumia na kufua na kuanika na tupo hai!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 02, 2014

    Wenzetu mlifua na kutumia na mko hai kwa sababu kwenu hakukuwa na uhaba wa maji. Kwa wenzetu maji hakuna, tena kwingine wasichana wanakosa kwenda shule kila wakiwa kwenye hedhi kutokana na hizo shida. Wakati "mpango wa utekelezaji wa kupeleka maji kwa hao watoto ukiwa mbioni" tunawapongeza wafadhili kwa kuona umuhimu wa kusaidia watoto wa kike kwenda shule kila siku ya shule mwezi mmoja.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 02, 2014

    Kweli mila zetu zimeingiliwa, vitu kama hivyo havijadiliwi hadharani kama hivi. Mwe kweli kuishi kwingi kuona mengi.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 03, 2014


    Anonymous wa May 02, 2014:

    Kuna ubaya gani..kuzungumzia usafi kwa wasichana, dada au mama zetu!

    Komboa ubongo wako; wewe ndio kikwazo!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...