Mtaalamu wa nyasi bandia kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Ian McClements amewasili Bukoba leo hii Asubuhi kwa Ndege ya kukodi.
McClements akiwa hapa Bukoba amekagua Uwanja wa Kaitaba, na baadae amekwea tena ndege yake kuelekea jijini Mwanza kukagua Uwanja wa Nyamagana.
Viwanja hivi vinawekwa nyasi bandia kwa ufadhili wa FIFA chini ya mpango wa misaada wa Goal Projects. Baada ya ukaguzi huo, McClements atatuma ripoti yake FIFA ili shirikisho hilo liweze kuteua mkandarasi wa kufanya kazi hiyo.
Kwa Tanzania viwanja vilivyowekwa nyasi bandia hadi sasa kupitia Goal Project ni Uwanja wa Uhuru uliopo Dar es Salaam, Uwanja wa Karume (Dar es Salaam) na Uwanja wa Gombani uliopo Pemba.
Kwa kuwa udongo wetu wa BK unastawi hadi (ndizi), (kahawa) na majani marefu wanamo zaliwa (senene) sidhani kama Nyasi za kueleta sifa za Uwanja bora wa Mpira Kiwango cha Fifa utakwama!
ReplyDeleteNitamshauri Baba Isaya Fred Felix Minziro tuihame Yanga S.C na kurejea Timu ya Nyumabni BK!
Mtatupata vipi kwa nini tusihamie Kagera Sugar?
UKOLONI KAMA KAWA
ReplyDeleteIvi kwa hali ya hewa ya bukoba, mbeya, morogoro, iringa, arusha na hata kigoma sidhani kama tunahitaji mawigi bandia.....natambua mikoa ambayo ipo ktk mradi huu, nimetaja mikoa hiyo kwakua natambua kwa hali ya hewa ilipo twaweza kuza nyasi na zikastawi na kupendeza, sielewi kwanini huwa tunapenda njia za mkato zenye kutugharimu kiasi hiki, ninaposema kutugharimu simaanishi fedha maana yawezekana FIFA imejitolea hapa namaanisha uoto wa asili na ecology.......
ReplyDeleteKwa hali ya hewa ya Bukoba sidhani kama tunahitaji nyasi za plastic. Tujiepushe na mambo ya kuiga. Kwa nini tusipande ukoka wetu wenyewe na kuajiri vijana wa kumwagilia.
ReplyDelete