Na Dixon Busagaga,Hai. 


WANANDOA wawili wameuawa kinyama baada ya mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Yusuf Njau (32),  anayeaminika kuwa ni mtoto wa wanandoa hao, kuwacharanga kwa shoka kisha kuchoma moto nyumba  yao na kutokomea kusiko julikana.
  
Tukio hilo la kusikitisha na la aina yake limetokea juzi majira ya saa 12:30 jioni katika kijiji cha Masama-Roo,  Kata ya Machame Mashariki,
wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro baada ya kijana huyo kuchukua uamuzi huo ambao unadhaniwa ni sababu za ugomvi wa kifamilia. 

Waliouawa wametambulika kwa majina ya Shahidu Njau(60) ambaye  ni baba yake mzazi wa mtoto huyo na  Minae Swai (57) ambaye ni mama mzazi wa mtoto huyo ambao kwa pamoja waliuawa baada ya kupigwa na shoka katika maeneo mbalimbali ya mwili. 

Kwa mujibu wa Taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa kijiji hicho, Halfani Swai alisema walipofika katika eneo la tukio baada ya kusikia ukunga, walikuta watu wakizima moto huku mwili wa Mama yake muuaji uliocharangwa na mapanga kila mahali ukiwa chini. 

Alisema kuwa wakati kijana huyo akiendelea kutenda unyama huo, alitokea baba yake mzazi, Mzee Shaidu  aliyekuja kuingilia kati ugomvi wa Mama na mwanae lakini naye alikatwa kichwani. 

Swali alisema Mwili wa Baba ulikutwa ukiwa pembeni wa mwili wa Mama ukiwa umekatwa kichwani na ubongo kufumuliwa lakini hata hivyo alikuwa bado hajafa. 

Alisema walimchukua kwa nia ya kuokoa uhai wake lakini muda mfupi baada ya kutoka kwenye eneo la tukio wakiwa katika kituo cha mafuta maeneo ya kwa Sadala Shaidu alipoteza maisha. 

"Tulikuta mwili wa Baba ukiwa pembeni nao ukiwa umejeruhiwa vibaya kichwani, ubongo ulikuwa pembeni, tulimchukua kumpeleka Hospitali lakini tulipofika kwa Sadala alipoteza maisha," alisema Swai.
 
Taarifa kutoka katika kijiji hicho zilisema muuaji, Yusuf Njau, ambaye amewahi kujifunza ngumi akiwa Dar es salaam amewahi kuwatishia Uhai baadhi ya ndugu zake zaidi ya mara mbili. 

Akizungumzia hali hiyo, Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Halfani Swai alisema kuwa kijana huyo ambaye ni morofi sana aliwahi kutishia kuwaua Shangazi na Baba mdogo.



"Muuaji aliwahi kuwatishia shangazi yake na Baba mdogo,amewahi kujifunza Ngumi na ni mkorofi sana kijijini kwake," alisema Swai.



Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Robert Boaz alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema mtuhumiwa huyo katika tukio la kutishia kuuwa shangazi na Baba Mdogo alikatwa na kuachiwa. 

Alisema kuwa miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya wilaya ya Hai ambapo juhudi za kumsaka Muuaji anayedaiwa kuonekana akiranda
kijijini hapo zinaendelea. 
 


Kwa upande mkuu wa wilaya ya Hai Novatus Makunga alisema tukio hilo ni kinyama na kuwataka wananchi kuwa na subira huku akitahadharisha raia kuchukua hatua mikononi. Makunga aliwataka Wananchi kuwaachia watu wa usalama kuchukua hatua huku akitahadharisha kuhusu jaribio la wananchi kuchukua hatua mikononi kuwa inaweza kuleta madhara zaidi. 

Wakati huo miili ya marehemu imezikwa jana mchana majira ya saa 7, kwenye makaburi ya Nyumbani, katika kijiji cha Masama Roo, Tarafa ya Masama, |Kata ya Machame Mashariki, wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 11, 2014

    Inna lillahi wa inna ilayhi rrajiuun
    (kilichotoka kwa Mwenyezi Mungu kitarejea kwa Mwenyezi Mungu)

    Jamani wanafamilia poleni sana kwa msiba huu wa aina yake.

    Tafadhalini wekeni picha ili muuaji huyu aweze kukamatwa po pote atapopatikana.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 11, 2014

    Poleni sana wanafamilia, tunawombeeni. Mwenyezi Mungu anawalindeni. Amani na upendo uwapoozi katika kipindi hiki cha majonzi. Mungu awarehemu walio tutangulia.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 11, 2014

    Inauma sana jamani, hii roho imetoka wapi? Mungu tusaidie. Mungu awape faraja wanafamilia na wote walioguswa na msiba huu mkubwa. Ni vema sasa labda tuanze kuchukua hatua mtu akianza kusema maneno ya kuua kwani inalekea anakuja kutekeleza, poleni sana.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 11, 2014

    Kuna nini huko Masama na yule muuaji wa ilala kwao ni hukohuko. Kuna tatizo la ukichaa hapo...polisi fanyeni uchunguzi

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 12, 2014

    wachaga wamekuwa wakibadilika na kuwa roho ya uuaji sijui kwann labda watuambie wenyew kama humu wapo.
    tukikumbuka tukio la ufoo saro na yule wa ilala. wote ni wachaga.
    kulikoni wachaga???????

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...