Kila Tar 18 Mei Jamii husherekea siku ya Makumbusho Duniani, hapa
Tanzania sherehe hizi Kitaifa zitafanyika Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar
Es Salaam. Katika siku hii muhimu, Makumbusho ya Taifa inatarajia kuufungua
rasmi Ukumbi wa Maonesho ya kudumu ya Sanaa.
Kutokana na umuhimu wa siku hii Makumbusho ya Taifa inawakaribisha
Watanzania wote kutembelea Makumbusho ya Taifa ili kujifunza mambo mbali mbali
kupitia vitu na naarifa zinazothaminiwa na jamii zilizo hifadhiwa na
Makumbusho.
Ufunguzi unatarajiwa kuanza saa 10 :00 jioni na utapambwa na Kikundi cha Sanaa cha GODYKAOZYA & THE TONGWA ENSEMBLE
kutoka Bagamoyo.
Kuanzia Tar 16 - 18 watu wote
watapatiwa huduma za Kimakumbusho BURE.
Usikose fursa hii Muhimu kwa ongezeko la uelewa wako juu ya nchi
yako.
Makumbusho ya Taifa na Nyumba
ya Utamaduni ipo Posta mtaa wa Shaaban Robert mkabala na chuo cha usimamizi wa
Fedha(IFM)
Karibuni sana.
SIXMUND
J. BEGASHE
MRATIBU
WA MAANDALIZI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...