Jhikoman aliwasili Finland tarehe 24.4.2014 kuanza ziara ya kimuziki katika nchi za Ulaya 
Nchini Finland amefanya maonyesho sita! Kubwa ni lile alilolifanya Helsinki African Film Festival 16.5.2014 
Pia alifanya onyesho la utangulizi kabla ya mkongwe Peetah Morgan wa Morgan Heritage kupanda jukwaani 23.5.2014. 
Tarehe 10.5.2014 alifanya onyesho kwenye uzinduzi wa Helsinki African Film Festival! 
 Jhikoman amefanyakazi studio na msanii mashuhuri wa Hip hop nchini Finland Paleface! Kwa sasa Jhikoman yupo studio akiandaa nyimbo aliyo mshirikisha Peetah Morgan. 
Tarehe 4 june 2014 Jhikoman anategemea kutumbuiza Kwenye ukumbi wa Nordic Black Theater mjini Oslo nchini Norway. Jhikoman pia anatarajia kudhuru miji ya Brussels Ubeligiji, Paris Ufaransa, Tübingen Germany, Stockholm Sweden na Copenhagen Denmark
Jhikoman and Peetah Morgan
Jhikoman akifanya majambo jijini Oslo
Akiwa studio na Paleface
Jhikoman akikamua ughaibuni
Jhikoman akiongoza mashambulizi Finland
Mwanamuziki Nyota wa Jamaika Peetah Morgan 
alikuwa jukwaani na Jhikomanhikoman

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 01, 2014

    Kweli Nabii huwa hathaminiwi myumbani kwake!HUyu ndio msanii anakuja Ughabuni na anafanya maonyesho live na bendi na sio wasanii wetu wa kuzuga wanofanya play back na c-d na kwenye ukumbi wa sebule za Wabongo.

    Ndoto ya Mchana Ughaibuni

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...