Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Kebwe S. Kebwe akizungumza na Menejimenti ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya alipotembelea Makao Makuu ya Mfuko huo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Balozi Ali Muchumo akitoa salaam za Bodi kwa Naibu Waziri.
Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Hamis Mdee akitoa maelezo ya awali na Taarifa ya utekelezaji ya Mfyuko.
Sehemu ya Mameneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya wakifuatilia taarifa ya utekelezaji iliyosomwa na Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko.
Baadhi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya wakisikiliza kwa makini maelekezo ya Naibu Waziri.
Mkurugenzi wa Mifumo Habari wa NHIF, Ali Othman akielezea namna Mfuko ulivyojipanga kutumia teknolojia kudhibiti udanganyifu.
Naibu Waziri akiteta jambo na Maofisa wakuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya baada ya kumaliza mazungumzo na Menejimenti.
Jipangeni kudhibiti udanganyifu. Watumiaji wa huduma na wafanyakazi wa mfuko tunahitaji kuwa waaminifu ili mifuko hii inayotoa huduma na ajira nchini kote iweze kudumu.
ReplyDeleteKuibia mwajiri wako ni kama kutotaka kazi yako iendelee. Akifilisika atafunga ofisi akifunga na wewe utakuwa huna kazi. Sasa faida iko wapi.