"Niliamini kuwa itatuchukuwa muda mrefu kusafiri kuweza kujenga na kutengeneza kitu ambacho kitatambulika kitaifa kitakuwa na heshima inayostahili na kitatoa mchango unaostahili na kitashawishi wachimbaji wengine kuona kwamba hii ni Fursa ambayo hakuna yeyote yule anayeweza kuiacha ipite pembeni. Sasa wacha niwapongeze NSSF kwa kuwa wajanja kati ya mifuko mingine yote ya jamii na kuamua kuliangalia kundi hili ambalo nguvu yake ya baadaye italiongoza taifa kuwa na matajiri wake wa ndani nikimaanisha wawekezaji wa ndani wenye nguvu Mabilionea"  alisema Naibu Waziri wa Nishati na Madini Steven Masele.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la taifa la Hifadhi ya jamii NSSF Crescentius Magori akizungumza wakati wa semina iliyoandaliwa na NSSF kuhusu mfuko huo kwa wachimbaji wadogo wa madini iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano Victoria Palace Hotel Capripoint jijini Mwanza.. 
Meneja kiongozi wa Mfuko wa Hifadhi ya jamii NSSF mkoa wa Mwanza akitoa maelezo ya awali na kutambulisha wadau mbalimbali walio hudhuria Semina kwa wachimbaji wadogo wa madini iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano Victoria Palace Hotel Capripoint jijini Mwanza, ikiandaliwa na NSSF.
Wadau wa NSSF wakinukuu pointi za msingi katika Semina ya wachimbaji wadogo wa madini iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano Victoria Palace Hotel Capripoint jijini Mwanza.
Naibu waziri wa wizara ya Nishati na Madini nchini Steven Masele ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi akizindua Mpango maalum na kufungua Semina kwa wachimbaji wadogo wa madini iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano Victoria Palace Hotel Capripoint jijini Mwanza. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...