Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akifungua kikao cha kupitia taarifa ya Uandishi wa Ripoti za Kina (Thematic reports) zinazotokana na Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 kutoka kwa watalaam mbalimbali wa Wizara, Idara na Taasisi za Serikali kilichofanyika leo katika Hotel ya Peacock Jijini Dar es Salaam.
Mshauri mtaalam wa Sensa ya Watu na Makazi Bw. Collins Opiyo kutoka Shirika la Kimataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani akitoa ushauri wakati wa kikao cha kupitia taarifa ya ripoti hizo kilichofanyika leo katika hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam.
Wataalam wanaoandika Ripoti za Kina (Thematic reports) kutoka Wizara, Idara na Taasisi mbalimbali za Serikali wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa (hayupo pichani) wakati wa kikao cha kupitia taarifa ya ripoti hizo kilichofanyika leo katika hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam. (PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO)
Hizo ripoti zikionyesha matatizo tuliyonayo zinafanyiwa nini? Wizara na wilaya mbalimbali zinazifanyia kazi au zinasaidiaje maendeleo?
ReplyDelete