.jpg) |
Akiwa ziarani Burundi,Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum) Profesa Mark Mwandosya (wa tatu kulia) ,amepata nafasi ya kutembelea Bandari ya Uvira,Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.Amepewa maelezo na Bwana Pierre Kalala Shabani,wa pili kulia. kuhusu shughuli za bandari hiyo ambayo ni ya pili kwa ukubwa baada ya Matadi.Wengine ni viongozi wa idara za bandari ya Uvira.Wamelalamika kudorora kwa shughuli za bandari kutokana na kupungua kwa ufanisi wa Reli ya Kati Tanzania. Waziri Mwandosya aliwapa maelezo kuhusu juhudi za Tanzania za kuendeleza reli ya kati,bandari ya Kigoma,na kiwanja cha ndege cha Kigoma.
Katika makaburi ya Mashjaa wa Burundi,Waziri na Mama Mwandosya watoa heshima zao kweye kaburi la Pierre Ngendandumwe aliekuwa Waziri Mkuu wa Burundi kati ya mwaka 1963 na 1965 ambaye aliuawa tarehe 15 Januari 1965. |
.jpg)
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum) Profesa Mark Mwandosya na Mkewe mama Lucy Mwandosya wakitoa heshima kwenye kaburi la Louis Rwagasore aliyekuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Burundi aliyeuawa Oktoba 1961
Waziri Mwandosya akutana na maafisa kutoka kiwanda cha saruji cha Mbeya Cement na mawakala wa Mbeya Cement Burundi.Waziri Mwandosya aliwapongeza Mbeya Cement kwa kuwa wauzaji wakubwa wa saruji Burundi.Aliwahimiza kuongeza juhudi kupanua soko Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Kutoka kushoto ni Ephraim Kalinga,Meneja wa Mauzo ya nje Mbeya Cement,Waziri Mwandosya,Emil Sindato ,Meneja Ufundi Mbeya Cement, Debrah Hernandez,mwakilishi wa wakala,na Eric Aneca,mwalikilishi wa wakaala wa Mbeya Cement.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...