Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua
Bwana Rished BADE kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Kulingana
na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, uteulzi huu umaanza tarehe 06 Mei,
2014. Bwana BADE anachukua nafasi iliyoachwa
wazi na Bwana Harry KITILYA ambaye alistaafu tarehe 14 Desemba,2013.
Kabla
ya uteuzi huo, Bwana BADE alikuwa Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania
tangu Septemba,2012 na baadaye kukaimu nafasi ya Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya
Mapato Tanzania tangia Bwana Kitilya alipostaafu.
Kabla
ya kujiunga na Mamlaka ya Mapato Tanzania, Bwana Rished BADE amewahi kufanya
kazi katika maeneo mbalimbali yaliyompa ujuzi na weledi mkubwa kwenye mambo ya
fedha na mapato kama ifuatavyo:-
Ø Oktoba,
1995 – Mei, 2000 – Mkaguzi wa Benki za Biashara, Benki Kuu ya Tanzania.
Ø Juni,
2000 – Juni, 2001 – Credit Manager, Akiba Commercial Bank.
Ø Juni,
2001 – Septemba,2001 – Chief Financial Officer, Akiba Banking Corporation.
Ø Septemba,
2001 – Machi, 2006 – Chief Operating Oficer, Barclays Bank (Uganda).
Ø Januari,
2007 – Desemba, 2009 – Chief Executive Officer, Barclays Bank (Tanzania)
Ø Desemba,
2009 – 2012 – Chief Financial Officer, (East and West Africa Cluster) Barclays
Bank Plc Emerging Markets.
Ø Novemba,
2010 – Septemba, 2012 – Chief Executive Officer, Tanzania Mortgage Refinance
Company.
Bwana
Rished BADE ana Shahada ya Kwanza ya Bachelor of Commerce and Management ya
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (1995); Shahada ya Master of Commerce in Banking
and Finance ya Chuo Kikuu cha Sydney (1999), na ni Certified Public Accountant
(CPA).
Katika
kumteua kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Mheshimiwa Rais ana
imani kubwa kwa elimu, uzoefu na weledi alionao, Bwana Rished Bade kwa
kushirikiana na watumishi wenzake, atatoa mchango mkubwa kwa Taifa kwa kuzidi
kuimarisha Mamlaka hiyo na kuboresha utendaji wake na hivyo kuongeza mapato ya
Serikali kwa faida ya Taifa.
“Mwisho”
Imetolewa
na:
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu
- Dar es Salaam.
08
Mei, 2014
.... congrats bro! i expect more v+ changes in TRA!!
ReplyDeleteHongera sana Ndg Bade. Tunakutakia heri simamia ukusanyaji wa mapato. Yaongezeke tuimarishe huduma kwa Watanzania.
ReplyDeleteRished hongera sana. Tunaomba uwe mkali uwafukuze wale wafanyakazi woote wa tra wanaopenda sana rushwa. Kuna wafanyakazi wa tra wanaoshi maisha ya hali ya juu. Mfano wamejenga majumba makubwa ya kifahari na pia kuwa na magari ya kifahari je pesa wamepaata wapi?? Na hao majamaa ni wadogo ni young graduates je pesa wanapata wapi kama siyo rushwa kuikosesha taifa mapato??? Fanyia kazi rished.
ReplyDelete