Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea shada la maua mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Nnamdi Azikiwe jijini Abuja, Nigeria, usiku wa Mei 6, 2014 ambako atahudhuria Mkutano wa siku 3 wa Uchumi Duniani kuhusu Afrika (World Economic Forum for Africa).
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Waziri wa Nishati wa Nigeria Profesa Chinedu Ositadinma Nebo na Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mhe Daniel Ole Njoolay katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Nnamdi Azikiwe jijini Abuja, Nigeria, usiku wa Mei 6, 2014 ambako atahudhuria Mkutano wa siku 3 wa Uchumi Duniani kuhusu Afrika (World Economic Forum for Africa).
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mhe. Daniel Ole Njoolay, Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Abdallah Kigoda na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,Mhe. Mohammed Aboud Mohammed baada ya kuwasili jijini Abuja, Nigeria, usiku wa Mei 6, 2014 ambako atahudhuria Mkutano wa siku 3 wa Uchumi Duniani kuhusu Afrika (World Economic Forum for Africa). 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 07, 2014

    Thank you Mr.President !

    Thanks to Tanzania Government!!!

    Nimefarijika sana kuona Mheshimiwa Dakitari Jakaya Kikwete anawasili Abuja kwa Presidential jet!

    Ndege ina Alama kuu kama:

    1.Nembo ya Adam na Hawa ya kuitambulisha Tanzania.

    2.Bendera ya Taifa.

    3.Jina la nchi 'UNITED REPUBLIC OF TANZANIA'.

    Hata wewe Mlalamikaji na Mpingaji ukibahatika kuwa Raisi wa nchi yetu tutahakikisha na wewe unasafiri na Presidential Jet!.

    Hapata kosa wa kulalama kwa kusema kwa hali tuliyo nayo hatustahili kumuhudumia Raisi wetu kwa ndege Maalum ya Raisi, tutambue Tanzania imekuwa na imeimarika kwa muonekano wake Kimataifa hivyo si busara kumsafirisha Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Commercial Airlines (Raisi kusafiria kwa ndege za kibiashara za abiria za kawaida)

    ReplyDelete
  2. JK na WEF ni kama nyuki na asali.. Safi sana Mh Rais. Ni heshima kubwa viongozi wetu waki-alikwa na kuhudhuria mikutano muhimu kama hivi.

    Ankal, naomba kama utaweza kutupigia picha ya aide-de-camp (ADC) mpya wa Rais wetu na ukiweza ku-zoom nametag yake ili tuweze kujua jina yake. Kwa wale amabo hawajui: ADC aliemtangulia amepandishwa cheo kuwa Brigedia na kwa hiyo amerudi jeshini. ADC kwa kawaida hutoka cheo cha Kanali..

    @Ndugu_Ali

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 08, 2014

    Ni matumaini tosha kuona Raisi wetu anasafiri kwa kutumia Presidential Jet!

    Tusiwe kama nchi mbili ndogo jirani ambazo tumeingia kuto kuelewana nazo huku zikiwa taabani na Maraisi wake mmoja wa Lilongwe akiuza Presidential jet ili kupata Mtaji wa Kisiasa na mwingine wa Kigali akilazimika kusafiri kwa madege ya kibiashara baa daya Uchumi aliokuwa akitegemea wa Vita kuyumba!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...